HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

6 November 2012

MWALUSAKO ULIJIAMURIA MWENYEWE SWALA HILI AU ?

Klabu bingwa Afrika mashariki na kati Yanga imetangaza kuondosha ajira kwa watendaji wawili waliotangazwa jana na katibu mkuu wa klabu hiyo Laurence Mwalusako kutokana na kwamba tangazo hilo la kuwaajiri watendaji hao halikupata baraka za viongozi wake kwa maana ya kamati ya Utendaji ya klabu hiyo.

 Mwalusako aliutangazia umma kuwa klabu hiyo imewaajiri watendaji wapya wawili kwa nafasi za meneja wa timu na afisa habari pamoja na kumtangza Davis Mosha aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo kushika nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu hiyo.

Watendaji waliotangazwa hiyo jana ni meneja Shabani Katwila na Baraka kiziguto kama afisa habari wa klabu hiyo
Mosha aliunganishwa na wajumbe wajumbe Muzamil Katunzi pamoja na Beda Tindwa kuongoza kamati ya mashindano ya Yanga.
Hii leo akiongea na waandishi wa habari huku akitetemesha maneno Mwalusako alikiri kufanya kosa kwa kutangaza watendaji wa klabu ya Yanga bila kufuata utaratibu jambo ambalo lilizua hali ya sintofahamu kutoka kwa viongozi wa klabu hiyo na leo kumuagiza mtendaji huyo mkuu mbele ya waandishi wa habari afute ajira hizo mara moja jambo ambalo Mwalusako amelitekeleza.
Akiongea na waandishi wa habari Mwalusako alionekana kushindwa kujibu maswali ya msingi likiwemo swali la dhamana ya kutangaza watendaji hao aliipata wapi hiyo jana na nani aliyekutuma kuja kurekebisha kauli yako.
Taarifa kutoka kwa kiongozi mmoja wa juu wa Yanga zinasema Mwalusako alikurupuka na kujitokeza kwa waandishi wa habari bila kufuata utaratibu na kutangaza habari ambazo hajapewa na viongozi wake licha ya ukweli kwamba kumekuwepo na mchakato wa kusaka watendaji wa nafasi hizo mchakato ambao bado unaendelea.
Kigogo huyo wa Yanga amesema kitendo kilichofanywa na Mwalusako mbali ya kuwashangaza lakini pia kimewasikitisha

Rockersports 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers