HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 November 2012

HARAMBEE STARS NDANI YA MWAZA LEO


Timu ya taifa ya soka ya Kenya (Harambee Stars) inatarajiwa kuwasili jijini Mwanza leo asubuhi ikiwa na baadhi ya nyota wake wanaocheza soka Ulaya akiwamo Denis Oliech anayecheza Ufaransa kwenye klabu ya Marseille na Victor Wanyama wa Celtic ya Scotland.
 Taifa Stars na Harambee Stars zitakutana kesho katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na mechi hiyo inachezwa katika siku ya mechi za kirafiki zinazotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA).
 Awali, Stars inayojiandaa na michuano ya awali ya Kombe la Dunia ilicheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Botswana katika mchezo uliofanyika jijini Gabarone na kutoka sare ya magoli 3-3.
Harambee Stars inayofundishwa na Mfaransa, Henry Michel pia itakuwa na Ayub Timbe Masika, ambaye anachezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, beki, Brian Mandela wa Santos ya Afrika Kusini na kipa, Anord Origi Otieno kutoka timu ya Ull/Kisa ya Norway.

Pia yuko kiungo wa zamani wa Simba ambaye sasa 'anakipiga' Coastal Union ya Tanga, Jerry Santo huku wachezaji wa ndani wakiwa ni Patrick Oboya, Mzee Patrick Ooko Osiako, Fredrick Jerim Onyango Oduor, Edwin Simiyu Wafula (AFC Leopards) na Eugene Ambuchi Asike (Sofapaka).

Wengine ni Geofrey Kokoyo Odhiambo, Mulinge Ndeto, Christopher Wekesa Nyangweso, James Wakhungu Situma (Sofapaka), Peter Odhiambo Opiyo, Charles Elphas Okwemba, Francis Kahata Wambura (Thika United), Andrew Kiriro Tololwa, Osborne Monday (Sofapaka), Wesley Kemboi na Moses Arita.

 Wakati huo huo, wachezaji wanne wa Taifa Stars wanaoichezea Yanga, Kelvin Yondani, Simon Msuva, Frank Domayo na Athumani Iddi 'Chuji' waliripoti katika kambi ya timu hiyo jana mchana na jioni walifanya mazoezi ya pamoja na wenzao kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo.
Nyota hayo walichelewa kutokana na kuwa jijini Tanga wakiitumikia timu yao katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Coastal Union uliofanyika juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambao walishinda 2-0.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers