HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

2 November 2012

MAAFISA KUMI WAFUNGIWA ZIMBABWE KWA UPANGAJI WA MATOKEO HUKU Norman Mapeza AKISUBIRI KAMA ATAHADHIBIWA



Norman Mapeza
Chama cha soka cha Zimbabwe  (Zifa) kimewafungia maafisa waanne kwa miaka kumi katika hukumu iliyotolewa muda mchache uliopita kwa upangaji wa matokeo  lakini kocha wa zamani wa Warriors  Norman Mapeza na wenzake 74 bado wanasubiri kama watapikana na hatia ili nao waingie katika mkasa wa adhabu.

Wote ambao wanatarajiwa kukumbwa na adhabu ya miaka mitano au pungufu ya hapo watatajwa baadae mwezi huu 
 . Jumla ya wachezaji Miamoja na maafisa bado wanafanyiwa uchunguzi kwa makosa ya kupokea fedha ili wapoteze mchezo katika ziara waliyofanya katika bara la Asia  mwaka 2007 and 2009. 

 Hadi sasa ni wachezaji kumi na tano na baadhi ya waamuzi wameshapataiwa adhabu za kufungiwa maisha na wengine nane bado wapo kando kupisha uchunguzi unaoendelea . 
Maafisa watatu kati ya wanne wamefungiwa maisha ambao walikuwa wanachezea klabu ya 
 Monomotapa, ambao walijifanya wachezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo katika ziara huko Malaysia  2008. 

 Rias wa Zifa  Cuthbert Dube ametangaza kuwaacha wachezaji wa wariors  ambapo walifungwa na Angola katika kufuzu kuwania kushiriki michuano ya mataifa ya afrika yatakayo fanyika  Afrka kusini  2013 
Japokuwa kocha  Rahman Gumbona msaidizi wake  Peter Ndlovu na  David Mandigora wameachwa kando katika kesi hiyo 
 Zimbabwe waliongoza  3-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza lakini walitolewa katika sheria za goli za ugenini baada ya kuruhusu magoli katika dakika sita za mwisho  

 Aliongeza kwa kusema kuwa wachezaji watakao chaguliwa tena katika mechi zijazo hawatoka katika wale waliopanga matokeo

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers