kampuni ya kutengeneza filamu za kitanzania yenye makao yake makuu sinza jijini dar es salaam ya RUFEDHA FILM hatimaye yazindua filamu yake ya kwanza ijulikanayo kama MORE THAN LIAR inayojumuisha mastaa kibao wa bongo move akiwemo mzee chilo na mainda.
uzinduzi huo umefaniyika katika ukumbi wa kilimani mjini dodoma jana na kuhudhuriwa na waziri wa habari,vijana,utamaduni na michezo mh DR FENERA MUKANGARA aliyekuwa mgeni rasmi,akizindua filamu hiyo mh mukangara waziri wa habari,vijana utamaduni na michezo amewataka wasanii nchini kutengeza filamu zenye mahadhi ya utamaduni wa mtanzania na kuwaasa wasanii kuongeza zaidi elimu zao za sanaa ili kuwa na ufanisi zaidi katika tasnia hiyo ya filamu.
naye mkurugenzi wa kampuni hiyo bwana salehe amempongeza mh waziri huyo kwa moyo wake wa kujitoa katika kuhamasisha sanaa hapa nchi na kuahidi kushirikiana naye hasa katika kudhibiti wizi wa kazi za wasanii hapa nchini huku akiipongeza kampuni ya mabibo beer kupitia kinywaji chake cha WINDHOEK na CLIMAX kwa kudhamini uzinduzi huo.
miongoni mwa wasanii waliopamba uzinduzi huo ni pamoja na bibi mwajata,batuli,na willson makubi katibu wa shirikisho la filamu tanzania

No comments:
Post a Comment