Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) linatarajia kutangaza ratiba ya mechi za mashindano ya kuwania ubingwa wa Kombe la Chalenji 2012 ifikapo Jumatatu jijini Kampala, Uganda, imefahamika.
Mbali na ratiba hiyo, tayari CECAFA imeiteua timu ya soka ya taifa ya Malawi (The Flames) kuwa ndiyo timu pekee mwalikwa katika mashindano hayo yatakayofanyika kuanzia Novemba 24 hadi Desemba 8 mwaka huu jijini Kampala, Uganda.
Nchi nyingine ambazo ziliomba kushiriki michuano hiyo ni pamoja na Ivory Coast, Zimbabwe na Zambia.
Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye, alisema kwamba tayari wamefanya maamuzi ya kuiteua Malawi na mashindano hayo ya mwaka huu yatashirikisha nchi 12.
"Tumeichagua Malawi kushiriki mashindano ya mwaka huu na tunaamini italenga ushindani wa timu zetu wanachama wa CECAFA," alisema Musonye.
Katibu huyo aliitaja Burundi kuwa ni miongoni mwa nchi zitakazoshiriki michuano hiyo na kukanusha taarifa za awali zilizotolewa kwamba nchi hiyo imejiondoa.
Alisema kwamba hii ni mara ya pili kwa Malawi kushiriki mashindano hayo na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kinnah Phiri, alituma maombi ya kutaka kikosi chake kishiriki michuano hiyo ili kujiandaa na mechi za kusaka tiketi ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Dunia zitakachofanyika mwezi Machi mwakani.
Wenyeji Uganda (Cranes) iliyoko chini ya Kocha Mkuu, Bobby Williamson raia wa Scotland ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo.
Kikosi cha Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kitakachoshiriki fainali hizo kinatarajiwa kutangazwa wiki ijayo baada ya mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayochezwa Novemba 14 dhidi ya Kenya (Harambee Stars) kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba jijini Mwanza.
CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment