HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

6 December 2012

Eritrea YAJIWEKA PEMBENI CHAN


Shirikisho la  soka nchini Eritrea limetangaza kuwa halitashiriki katika mechi yao ya kuwania kufuzu kombe la mataifa ya  Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki katika ligi ya Nyumbani, dhidi ya Ethiopia.

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limethibitisha uamuzi huo, lakini halijatoa sababu yoyote ya kujiondoa kwa Eritrea.

Siku ya Jumanne, Shirikisho la  soka nchini Ethiopia, liliomba CAF, kupeleka mechi yao na Eritrea katika nchi tofauti, kwa kuwa nchi hizo mbili jirani, zinazozana kuhusu suala la mipaka.

Wachezaji 17 wa timu ya taifa ya Eritrea na daktari wao waliotoweka nchini Uganda siku ya Jumanne, wameomba hifadhi nchini humo.

Kamishna anayehusika na masuala ya wakimbizi katika ofisi ya waziri mkuu, David Apollo Kazungu, amesema   kuwa wachezaji hao wa Eritrea walimtembelea ofisi yake  kuomba kupewa hifadhi.

Apollo alisema kuwa wachezaji hao na afisa huyo walimueleza kuwa hali nchini mwao sio nzuri na kuwa ofisi yake inachunguza nyaraka zao kabla ya kuchukua hatua.

''wao wote watasalia chini ya serikali ya Uganda kwa kuwa wamesajiliwa rasmi'' aliongeza Bwana Apollo Kazungu.

Kazungu amesema wanashirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR, jinsi watakavyowasaidia wachezaji hao wa Eritrea.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers