HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

27 December 2012

Kumbe si soka tu Fabrice Muamba Ni Noma

Baada ya kunusurika kupoteza maisha  ndani ya uwanja, hali iliyompelekea kustaafu Kucheza soak  katika Umri mdogo, Fabrice Muamba ameonesha kipaji chake katika Tasnia  sanaa ya kucheza Muziki katika kipindi maalumu cha dansi ‘Strictly Come Dancing’ kinachorushwa na Televisheni ya BBC Entertainment.

Ikiwa ni miezi kadhaa tangu kustaafu Mpira wa miguu, Muamba mwenye miaka 24 alicheza wimbo maalum wa Christmass ‘The Waitresses’ katika mtindo wa Salsa huku akipewa sapoti na dansa wa kike maarufu kama Vilani.

Mchezaji huyo wa zamani wa Bolton Wanderers na mzaliwa wa Congo, aliwambia waandishi wa habari kuwa lengo la yeye kushiriki ni kutaka kufurahi na kupata faraja, Muamba aliongezea “ ulikuwa ni uzoefu mzuri sana kwangu na nimefurahia, nilitaka kuonesha ulimwengu upande mwingine kuhusu mimi, pia ni jukwaa la kuonesha kuwa sasa nafanya vingine”.

Muamba alimalizia kwa kusema “ Ndio! nakumbuka sana kucheza mpira lakini ipo wazi sababu ya kwanini sitocheza tena, na kitu muhimu zaidi katika maisha yangu ni Mke wangu na mwanangu”.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers