HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

27 December 2012

LABDA KAMA WANAKIKAO CHA HARUSI NA SI VINGENEVYO :RAGE


Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Aden Rage ameupuuza Mkutano Mkuu wa baadhi ya wanachama wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam Jumapili kwa madai kwamba haujaandaliwa kwa kufuata katiba ya klabu hiyo.
 Rage amesema mkutano huo unaouitwa wa dharura ni batili kwa vile hata wanachama waliouomba, robo tatu yao ni wafu.

 “Nimepokea barua na orodha ya watu 698 wanaotaka Mkutano Mkuu wa Dharura ufanyike Desemba 30 (Jumapili) mwaka huu na mkutano huo ni batili kwa sababu haujazingatia katiba ya Simba,” .

“Katiba yetu (Simba) inasema mwenyekiti ataitisha Mkutano Mkuu wa Dharura baada ya kushauriana na kamati ya utendaji ya klabu au endapo wanachama hai wasiopungua 600 wataomba kuitishwa kwa mkutano huo.

“Tumepitia orodha ya wanachama waliojiorodhesha kutaka kuitishwa kwa mkutano huo na kugundua kuwa robo tatu ni wanachama wafu wa Simba (hawajalipa ada ya uanachama).”

Alisema kuwa chochote kitakachojadiliwa na watu watakaohudhuria mkutano huo kuhusu Simba hakitafanyiwa kazi na kamati ya utendaji ya klabu hiyo kwa kuwa mkutano huo uko kinyume na katiba yao.

 "Kama watakutana Desemba 30, nafikiri watakuwa kama wanaojadili masula ya harusi ama msiba maana masuala ya Simba hayawezi kujadiliwa katika mkutano ambao si rasmi," alisema Rage.

Kwa mujibu wa katibu wa jopo linaloratibu mkutano huo, Mohamed Wandi, wanachama 698 wa klabu hiyo wanatarajia kukutana Jumapili kujadili mustakabali wa klabu yao.

Wandi alikaririwa akisema wanakutana kujadili mwenendo mbovu wa timu yao katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambapo timu yao ilimaliza ikiwa katika nafasi ya tatu.

Wandi alisisitiza kuwa wanakutana kwa matakwa ya katiba ya klabu yao Ibara ya 22 kifungu cha (ii), hivyo ni mkutano halali uliokidhi vigezo kikatiba.

Simba, ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, wamekuwa na misuguano baada ya timu yao kufanya vibaya katika mechi za kuelekea mwishoni mwa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.

Katika hatua nyingine, Rage alisema kuwa itaondoka nchini Januari 10 kuelekea Muscat, Oman ambako itaweka kambi kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers