HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

26 December 2012

ONE FOR THE ROAD


Klabu bingwa nchini Kenya Tusker hii leo imefanikiwa kuifunga klabu bingwa Afrika mashariki na kati Yanga ya Tanzania kwa bao 1-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki ulikochezwa katika uwanja uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bao la Tusker lilipatika katika dakika ya 44 ya mchezo likifungwa na Ismail Dunga kwa njia ya penati baada ya mwamuzi wa mchezo huo Oden Mbaga kuamuru penati hiyo iliyotokana na kiungo Nurdin Bkari kumuangusha katika eneo la hatari Aucho Khali.

Katika mchezo huo Yanga inayofundishwa wa kocha wake Ernstus Brands iliwatumia wachezaji wake watatu iliyo waongeza katika usajili wa dirisha dogo akiwemo Kabange Twite na wachezaji vijana waliopandishwa kutoka kikosi cha pili Rehani Kibingu na George Banda ambao walionyesha uwezo wa kuridhisha licha ya kucheza kipindi cha kwanza kabla ya kutolewa mapumziko.

Kipindi cha pili licha ya Yanga kuwaingiza Hamisi Kiiza, Jerson Tegete, Omega Seme na Nizar Khalfan wakichukua nafasi za George Banda, Rehani Kibingu, Ladslaus Mbogo, Saidi Bahanuzi na David Luhende bado matokeo ya mchezo huo yalisalia kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza ingawa mabadiliko hayo yalibadilisha sura ya mchezo kwa Yanga kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Tusker katika dakika za mwisho wa mchezo huo.
Baada ya mchezo huo Yanga sasa inajiwinda na safari ya wiki mbili nchini Uturuki ikiwa sehemu yake ya maandalizi ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara, safari ambayo imepangwa kufanyika kabla ya mwaka mpya.

Tusker ilingara na wachezaji wake kama George Opiyo, Luke Ochieng, Joseph Shikokoti, Ismail Dunga na Robert Omonuk.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers