Timu ya soka ya Sao Paulo ya Brazil imepewa ubingwa kombe la Copa Sudamericana usiku wa kuamkia leo baada ya kutokea vurugu ndani na nje ya kiwanja baada ya timu kutoka Argentina Tigre kugoma kucheza kipindi cha pili cha mkondo wa pili wa fainali hiyo ambao huchezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini
Maafisa wa Tigre wamesema wachezaji wao walivamiwa na maafisa usalama wakati wa mapuumziko katika vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kutokea kutokuelewana mara baada ya kipindi cha kwanza kumalizika .
Kocha wa Tigre Nestor Gorosito alikuja kuwaeleza Wanahabari wakati wa mapuumziko Mlinda mlango wa wetu alinyooshwa silaha kifuani kwenye chumba cha kubadilishia nguo tumeamua kutokucheza tena hiki ni moja ya kielelezo kuwa wanausalama hawajatutendea haki
"Hatuchezi tena ."
Mwamuzi Enrique Osses kutoka Chile aliipatia ushindi Sao Paulo baada ya kusubiri kwa muda wa dakika 30 kuisubiri Tigre kurudi uwanjani .
Timu hizo mbili zilizozana baada ya nusu ya kwanza kumalizika Runinga kutoka Argentina ilionyesha picha kuwa kulikuwana ugomvi ambao haikuweza kufahamika kwa mara moja chanzo kilikuwa nini lakini ilionekana wazi vurugu zilikuwa kubwa .
No comments:
Post a Comment