HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

22 December 2012

TANZANIA 1 ZAMBIA 0

TIMU ya Taifa Stars ya Tanzania leo imeifanya vibaya timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo) baada ya kuifunga bao moja kwa bila. Zambia ambao ni mabingwa wa Afrika walipata kichapo hicho baada ya mshambuliaji wa kutumainiwa wa kikosi cha Stars Mrisho Ngassa kuifungia timu yake goli la kwanza katika dakika ya 45 kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza. Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa katika uwanja wa taifa wa Tanzania jijini Dar es Salaam. Stars walionekana kucheza kwa umakini na kwa kujihami tangu awali jambo ambalo liliwanyima nafasi kabisa wapinzani wao kuweza kupenya katika goli la Tanzania. Hadi dakika 90 zinamalizika Tanzania 1 na Zambia haijapata kitu.

Mshambuliaji wa Taifa Stars,Mrisho Ngassa akijiandaa kuachia shuti kali lililoipatia Stars bao la kuongoza wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imeshinda bao 1-0.

Kocha wa Taifa Stars,Kim Poulsen akipeana mkoni na Kocha wa Zambia ambaye alionekana kutofurahishwa na Matokeo ya kufungwa kwa Timu yake,mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar jioni hii.Taifa Stars imeshinda bao 1-0.

Mshambuliaji wa Taifa Stars,Hamis Mcha (katikati) akiwachachafya mabeki wa timu ya Zambia katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa stars imeshinda bao 1-0.




No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers