HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

30 December 2012

YANGA YAWASILI Antalya IIKITOKEA Istanbul

Kikosi cha mabingwa wa kombe la Kagame mara mbili mfululizo timu ya Young Africans imewasili salama katika mji wa Antalya kusini mwa nchi ya Uturuki majira ya saaa 10:30 jioni kwa saa za afrika mashariki na kati na moja kwa moja kupolekewa na wenyeji wake kampuni ya Team Travel.

Young Africans imefikia katika hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kilomita chahce kutoka katika uwanja wa ndege wa antalya, ambapo hoteli ya Fame Residence ipo mwambaoni mwa bahari ya mediteranian.

Mwanzoni Yanga ilikuwa ifikie katika hotel ya Sueno Beach Hotel iliyopo kilometa 70 kutoka uwanja wa ndege lakini jana siku moja kabla ya safari ilifanya mabadiliko na ku
amua kuhamia katika hotel ya Fame Residence.




Wachezaji wamefurahi mandhari ya hotel kwani ni miongoni mwa hotel za nyota tano katika mjii huu wa Antalya hivyo wamefariijika na kuupa hongera uongozi kwa hatua waliyofikia ya kukubaliana na mwalimu kuweka kambi ya mafunzo nchini Uturuki.



Timu itaanza mazoezi kesho asubuhi katika viwanja vilivyopo katika eneo la hotel ya fame, ambapo kwa siku timu itakua inafanya mazoezi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni.

Kuhusu hali ya hewa ni baridi kiasi na sio baridi kali kama ilivyokuwa inatangazwa na vyombo vya habari hapo awali.

Mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz utaendelea kuwajuza juu ya kila kitu kinachojiri nchini Uturuki.
http://www.youngafricans.co.tz/

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers