Chama soka cha Zanzibar ZFA wiki hii
kiliwafungia wachezaji waliohusika kugawana fedha za ushindi wa tatu katika
mashindano ya Cecafa yaliyofanyika huko
Uganda na wenyeji kutwaa Ubingwa .
katika hari isiyoyakutegemewa chama hicho
kimewafungiwa Nadir Haroub Ali " Cannavaro, msaidizi wake Agrey Morris,
Khamis Mcha " Viali" Nassor Masoud " " Cholo" Twaha
Mohammed, Suleiman Kassim " Serembe" na Abdallah Seif kwa kosa la
kugawana fedha hizo wakiwa nchini Uganda Chama hicho kimewafungia Mwaka mmoja
wachezaji huku kikilitaka shirikisho la soka la Tanzania kutambua adhabu hiyo jambo
ambalo wadau wengi wametokea kulipinga na wengine kuliafiki K-SPORT.COM imeamua
kukusanya baadhi ya Data na kulitazama jambo kwa pande mbili za sarafu .
Upande wa kwanza ingekuwaje kama
kitendo hiki kingefanywa na wachezaji wa Tanzania bara Je tff ingeridhia na
kukiona cha kawaida ? jibu la haraka sio kweli hata kidogo Tanzania iliwahi kucheza na Cameron na
Nadir Ali alibadilishana jezi na Samuel Eto’o jambo lililozua gumzo nchini
kiasi kufikia baadhi ya wadau kulipa fedha hizo taslimu baada ya shirikisho kumtaka arejeshe jezi
pengine mungu alitaka kumtumia Nadir haroub kuonyesha kuwa wachezaji wetu
hurudia jezi moja au wanapea moja ya jezi kwa mechi zote .
Tuonavyo ilikuwa ni jambo la TFF na
ZFA kukaa pamoja na kujadiri swala hili
na sio kila upande kufanya wachofikiri ni sahihi – kwa upande mwingine ZFA ina haki kwani ni kitendo cha kuidharirisha taifa hili dogo lisilofahamika
katika soka ya kimataifa lakini likifahamika katika Ukanda wa afrika mashariki na kati huku likiwa
mwanachanma wa muda wa shirikisho la soka barani afrika CAF .
Yamkini ZFA walichotakiwa kufanya ni
kutazama aina ya adhabu kwani katika ulimwengu wa leo huezi kumfungia mchezaji
mwaka mzima kwa kosa la kugawana fedha wakati adhabu hiyo mara nyingi hutolewa
kwa makosa ya rushwa au kupanga matokeo hakika kwa hili ZFA inayohaki haki
kuwaadabisha wachezaji lakini sio kwa kiasi cha adhabu walichopewa ni adhabu kubwa kuliko mategemeo lakini kubwa zaid TFF inatakiwa kukaa chini na
kukemea swala hili sio swala la ZFA pekee kwani-;
leo inaonekana kama Zanzibar Heroes haipewi
heshima hata kidogo kwani si jambo jema
K-SPORT inazishauri ZFA kutumia hekima na kukaa chini na TFF kuheshimiana na
kujadiliana katika stahiki na nidhamu ya
vyama husika na kuwa na nidhamu katika kuheshimiana na wachezaji wawe na
nidhamu kutii na kuwajibika inavyotakiwa .
ZFA NA TFF KAENI CHINI PAMOJA
NIDHANU LAZIMA IZINGATIWE
No comments:
Post a Comment