Uongozi
wa chama cha Zanzibar ZFA Kupitia Rais wa ZFA Ibrahim makungu kimeshaliandikia Barua shirikisho la soka la Tanzania TFF ili kutekeleza adhabu za wachezaji tisa wa Zanzibar kufungiwa kwa mwaka kutokucheza soka nje na ndani ya Zanzibar na kupinga hoja ya kuwa ZFA haina ubavu wa kuwafungia wachezaji hao.
kwani ZFA imesema wao ni wanachama wa CECAFA na inauwezo kuwafungia wachezaji kwani kitendo hicho kimefanyika katika mashindano ya CECAFA na hivyo adhabu hiyo kuanza mara moja wachezaji hao wa Zanzibar Heroes waligawana fedha wakiongozwa na Nadi Haroub fedha hizo walizipata Mara baada ya kuifunga Tanzania Bara katika mashindano hayo, kama tff itaafiki basi wachezaji hao watafungiwa mwaka mzima .
ZFA imesema kuwa kitendo hicho cha wachezaji hao hakivumiliki na wametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine .
No comments:
Post a Comment