Manchester City imeanzisha mazungumzo na vilabu vya AC Milan na
Juventus kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wake Mario
Balotelli, na ripoti zinasema kuwa, Balotelli atauzwa ikiwa vilabu hivyo
vitaweza kulipa fedha wanazo taka.
Klabu
hiyo imesema mchezji huyo mwenye umri wa miaka 22, anakisiwa kugharibu
pauni milioni ishirini na moja mbali na fedha zingine za ziada.
Balotelli hana haraka ya kuuzwa na Manchester City imesema haina mipango ya kupunguza mshahara wake ili aondoke.
Kinyume na matarajio ya wengi Balotelli
amesafiri na wachezaji wa Manchester City watakaocheza na QPR katika
mechi ya ligi kuu ya premir leo usiku.
Milan ilianzisha mazungumzo na Man City, kuhusu
mchezaji huyo kutoka Italia na kuna ripoti kuwa klabu ya Juventus vile
vile imewasilisha ombi la kutka kumsajili Balotelli, ambaye alijiunga na
Manchester City Agosti mwaka wa 2010 kwa kitita cha pauni milioni 24.
Mapema siku ya Jumatatu, naibu kocha mkuu wa Man City, David Platt, alisema kuwa Balotelli hatajiunga na AC Millan mwezi huu.
Siku ya Ijumaa wiki iliyopita, kocha wa Man City
Roberto Mancini, alikariri hana nia ya kumuuza kuwa mchezaji huyo
kutoka Italia.
Balotelli ambaye amefunga goli moja baada ya kucheza mechi kumi na nne msimu huu, amekumba na kashfa nyingi tangu aliposajiliwa.
Tukio la hivi karibuni, likiwa mzozo kati yake na Mancini katika uwanja wao wa mazoezi mwanzo wa mwezi huu.
Makamu wa rais wa AC Milan Adriano Galliani
amesema ikiwa Manchester City itapunguza bei ya mchezaji huyo, basi
huenda wakamsajili.
No comments:
Post a Comment