Kocha wa zamani wa klabu soka ya Barcelona Pep Guardiola amezungumza kwa mara ya kwanza kuwa anataka kupata changamoto mpya kwa kufundisha klabu moja wapo nchini uingereza .
Guardiola, ambaye ameipatia Barca mataji 14 katika misimu minne anaonekna kutafuta kibarua kipya kwa sasa .
Pep 41 amesema kuwa akiwa kama mchezaji akufanya maamuzi ya kutaka kucheza soka uingereza lakini siku za usoni anatarajia kuwa mkufunzi katika soka la uingereza
."
Kwa maneno haya Man city ,Chel,na united timu ambazo zinaamini kuwa zinahitaji hasa saini ya mkufunzi huyo na zimekuwa zikimfuatilia Guadiola zinaweza kufanikiwa kumpata na hii inakuja mara baada ya Jose Mourinho kuonyesha dhahiri kuwa anataka kurejea uingereza
Guardiola aliongeza kwa kusema : " Ni kitu cha kipekee kucheza ligi hii .Nataka kuona hisia za mashabiki, Mzingira , Vyombo vya Habari aina ya wachezaji na kila kihusucho ligi ya Uingereza
kiukweli ni ligi bora ukizingatia mimi bado mdogo .
"
Guardiola Kwa sasa anaishi New York na familia yake baada ya kuamua kuchukua mapumziko ya mwaka mmoja
Loic Remy NA Yann M'Vila
Kocha wa Queens Park Rangers Harry Redknapp amesema kuwa Loic Remy amefaulu vipimo vya afya na sasa kinachofanyika ni makubariano binfsi kati ya yeye na klabu husika na amesma yuko karibuni kumtia kwapani kiungo wa ufaransa Yann
M'Vila.
Mshambuliaji wa Marseille Remy, 26,alionekana kwenda
Newcastle lakini sasa atajiunga na QPR kwa ada ya uhamisho wa pauni £8m, wakati kiungo wa Rennes
M'Vila, 22, anatarajiwa kuwagharimu pauni £7m.
Redknapp amesema alivutiwa kusainisha wachezaji ambao anaona wanaafaa kwa klabu yake
"na ameongeza kuwa anatarajia kumnasa mshambuliaji wa West Brom Peter Odemwingie kwani tumesha pereka maombi ya kumsajiri lakini inaonekana imezimwa na una haki ya kumuhitaji ni mchezaji mzuri kocha huyo bado anamsaka Mlinzi Jonas Olsson na Kiungo wa Tottenham Jake Livermore.
QPR waliifunga West Brom 1-0 na kuingia hatua ya nne ya michuano ya FA na kundelea na Takwimu ya kutokufungwa mwaka 2013
No comments:
Post a Comment