Mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos amepewa Adhabu ya Kufungiwa kwa mechi tano baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu hapo jana usiku katika michuano ya kombe la mfalme Ambapo timu yake iliifunga Celta Vigo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uispania alipewa adhabu hiyo katika dakika ya 72 baada ya kupewa kadi ya pili ya manjano na kuonyesha ishara kuwa mwamuzi hakumtendea haki pindi alipokuwa akitoka nje ya kiwanja .
Shirikisho la soka la Uispania limetangaza kuwa mchezaji huyo atatumikia adhabu ya mechi moja nje na atakosa mechi nyingine tano kwa mujibu wa Kifungu cha 94 RFEF's Cha nidhamu kinacho zungumzia maswala ya udhalilishaji kwa waamuzi au mtu yeyote .
Madrid ilishinda Mabao 4-0 na kufudhu hatua inayofuata ya robo fainali baada ya kushinda kwa jumla ya magoli 5-2 .
No comments:
Post a Comment