Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba wameanza Mazozei nchini Oman kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki mbili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu.
Simba iliondoka jijini juzi kuelekea Oman kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara na mechi za Ligi ya Klabu Bingwa Afrika.
Katibu mkuu wa Simba, Evodius Mtawala amesema wachezaji wote wako imara na wanaendelea vyema na mazoezi.
Simba imepanga kucheza mechi tatu za kirafiki kabla ya kurejea nchini kuanza mzunguko wa pili wa ligi na kwamba katika mechi ya kwanza wataikabili timu ya Fanja FC ya Oman.
Akizungumzia kuhusu kutolewa katika Kombe la Mapinduzi amesema hatua ya kupigiana penalti ni ya bahati kwa upande wowote.
"Kikosi kilionyesha uwezo mkubwa, lakini bahati haikuwa yetu," .
Aliongeza kuwa wanaipongeza Simba kwa hatua waliyofikia na kuwataka wachezaji wasivunjike moyo na kushindwa kufika fainali.
Aliongeza kuwa wameshaufunga ukurasa wa michuano hiyo na sasa wanajipanga kuwasafirisha wachezaji waliobaki kwenye michuano hiyo ili wakaungane na wenzao 14 waliotangulia kambini Oman.
Simba ambayo inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu itarejea nchini baada ya wiki mbili kwa ajili mzunguko wa pili wa ligi kuu inayotarajia kuanza mwishoni mwa mwezi katika viwanja tofauti nchini.
No comments:
Post a Comment