Ikiwa ni sehemu ya
udhamini wake, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi vifaa vya michezo
kwa klabu maarufu za Simba SC na Young Africans SC kwa ajili ya awamu
ya pili ya msimu wa 2012/13 wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki
hii.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro
Premium Lager, George Kavishe alisema “Bila shaka Simba na Yanga ndio klabu
kubwa zaidi hapa Tanzania
zikiwa kwa pamoja zimeweza kupata mafanikio makubwa kwa kipindi kirefu na bado
zinaendelea kufanya vizuri. Tunajivunia kuweza kuziunga mkono klabu hizi katika
jitihada za kuwania taji la ligi kuu
msimu huu.
Vifaa ambavyo leo
tunatoa ni pamoja na mipira, viatu, soksi, shin guards, nguo za mazoezi, nguo
za kawaida, gloves na vitu vingine vingi ambavyo vitawezesha timu hizi za Simba
na Yanga kucheza wakifurahia kuvaa vifaa vyenye ubora wa hali ya juu.
Kilimanjaro Premium
Lager kama mdhamini mkuu wa Simba na Yanga, na kinywaji kinachoongoza katika
udhamini wa soka hapa nchini tunadhani kwamba uhusiano wetu na klabu hizi ni
kiungo muhimu sana katika kuendeleza mpira wa miguu hapa Tanzania. Tutaendelea
kutimiza majukumu yetu kwa klabu hizi na kama ilvyo kawaida yetu, tutahakikisha
tunalifikisha soka la Tanzania
kwenye kilele cha mafanikio. kabisa
kwani, pamoja na uhusiano huo mzuri na klabu hizi mafanikio makubwa
yanatarajiwa katika kuendeleza soka la Tanzania.
Kavishe alisema kuwa ushirikiano
kati ya Kilimanjaro Premium Lager na klabu hizo umesimamia katika misingi ya
kufanya kazi pamoja, uadilifu na kuendelea kupata mafanikio. “Ushirikiano huu unasaidia
kukuza mpira wa Tanzania,
kuleta msisimko, na kuvutia mashabiki wengi wa mpira wakati na vilevile
kuwaweka wachezaji wa Tanzania
katika nafasi nzuri ya kimataifa.
Tunachukua nafasi hii
kuwashukuru viongozi wa Simba na Yanga walioko hapa, mashabiki wote, vyombo vya
habari na wadau wote wa mpira kwa ushirikiano mzuri tunaoendelea kupata kwenye
udhamini wetu na hiyo ndio siri ya mafanikio ya uhusiano wetu na klabu hizi
mbili maarufu.
“Tunaahidi ushirikiano
kwa klabu hizi nzuri na kama tunavyosema kila mara lengo letu ni kufikisha
mpira wa Tanzania kwenye ngazi za kimataifa na kuwafikisha mashabiki wa mpira
na wapenzi wa Kilimanjaro Premium Lager kwenye kilele cha mafanikio.”
No comments:
Post a Comment