Kocha wa Arsenal Raia wa ufaransa Arsene Wenger amesema "99%" anauhakika kuwa mshambuliaji wake Theo Walcott atasaini kandarasi mpya klabuni hapo mwishoni mwa juma hili ambapo mambo yatakuwa yamekamilika Walcot 23, ambaye yupo katika miezi sita ya mwisho klabuni hapo na anao uwezo wa kuondoka wakati wa kiangazi.
Laki ni wenger amesema kuwa kwa sasa ana asilimia 99 za kumbakisha mchezaji huyo .
"sikuwa na furaha pale niliposkia angeondoka "
"Imetuchukua muda kufika hapa tulipotaka bado hatujalimaliza lakini itakuwa tayarai ndani ya juma hili" .
Walcott ndio mfungaji anaeongoza kwa arsenal akiwa amefunga magoli 14 .
Mchezaji huyo alikataa kandarasi ambayo angepewa ujira wa pauni £75,000 lakini yeye alitaka kulipwa pauni laki moja kwa juma
Wenger bado anahusishwa na kutaka kumsajiri winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha, Mchezaji huyo Mwenye miaka 20 Aidha mfaransa huyo amethibitisha kutaka kumsajiri mchezaji ,
Taarifa zinasema kuwa
Arsenal wako mbioni kumsajiri mshambulijai wa Napoli mwenye miaka 25-Kutoka Uruguay Edinson Cavani.
huku akisema bei inaweza kupanda na ni jambo la kawaida lakini inaweza kupungua siku za mwisho au saaa kdhaa kabla dirisha kufungwa.
Petrov AMALIZA UHAMISHO WA KWENDA Espanyol
Martin Petrov Amekamilisha uhamisho wake kutoka katika klabu ya Bolton Kuelekea La Liga hasa katika klabu ya Espanyol, Klabu hiyo inayoshiriki ligi ya pili nchini uingereza imethibitisha
Kocha wa Botlon Dougie Freedman amekumbusha kuwa mchezaji huyo kutoka Bulgaria alikuwa akifanya mazungumzo mapema wiki hii na Barcelona-lakini mazungumzo hayo yamekamilika Rasmi kwa kujiunga na Espanyol
Petrov aliwahi kuchezea Nchi USpania akiwa na Atletico Madrid kabla hajakwenda Manchester City majira ya kiangazi 2007.
No comments:
Post a Comment