Mzunguko
wa pili ya Ligi Kuu ya Vodacom utaanza Januari 26 mwaka huu huku kukiwa
na maombi ya televisheni ya SuperSport kuonesha mechi za Super Week
kama ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza.
Raundi
tano za awali katika ratiba ya mzunguko wa pili zinabaki kama zilivyo
wakati nyingine zilizobaki zitatolewa baada ya kuingiza mechi za Super
Week.
Wakati
huo huo, mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza unatarajia kuanza
Januari 26 mwaka huu. Ratiba ya ligi hiyo na tarehe rasmi ya kuanza
itatangazwa baada ya kupitiwa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) inayotarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki.
No comments:
Post a Comment