WAGOMBEA
wanaowania nafasi za juu na ujumbe za uongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) na Bodi ya
Ligi Kuu wamewekewa pingamizi na wadau
mbalimbali wasigombee nafasi walizoomba.
Katibu Mkuu
wa TFF, Angetile Osiah ambaye ni Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF,
amewaambia Waandishi wa Habari kwamba, jumla ya pingamizi 14 zimewasilishwa
tangu zoezi hili lilipoanza na kuhitimisha jana.
Wagombea waliowekewa pingamizi ni Jamal Malinzi, Athumani
Nyamlani wanaogombea Urais wa TFF, Michael Wambura anayegombea nafasi ya makamu.
Pia Angetile
alisema kwamba upande wa Bodi ya Ligi Kuu, wagombea Yussuf
Manji, Ahmad Yahya Juma na Mohamed Said anayegombea nafasi ya makamu wamewekewa
pingamizi pia.
Aidha,
wagombea wa nafasi za Ujumbe, Epatha Swai, Eliud Mvella na Athumani Kambi
wamewekewa pingamizi.
Nyamlani
amewekewa pingamizi mbili, moja na Mtanga Yussuf Gacha na nyingine ya Menard
Justinian, wakati Malinzi amewekewa pingamizi moja na Agape Fuwe. Wambura yeye amewekewa
pingamizi mbili, moja ya Osiah Samuel Msengi na Saidi
Rubeya.
Wajumbe Epatha Swai
amewekewa pingamizi na Ramadhan Sesso na Sos Chalamila, Eliud Mvella amewekewa pingamizi na
Saidi Kiponza, Abdul Changawa na Peter Namengi, wakati Athumani Kambi yeye amewekewa pingamizi
na Jeremiah John Wambura
Manji
amepingwa na watu wawili ambao ni mwanachama maarufu wa Simba, Daniel Tumaini Kamna
na mwingine ni mwanachama wa Yanga, Juma Ally Magoma, Frank Mchaki amepingwa
Ahmad Yahya na Mohamed Said.
Kamati itakutana jumatano kujadili pingamizi hizo na inawakumbusha wote
waliowekewa pingamizi kufika ofisi za TFF saa 4:00 asubuhi siku hiyo kusikiliza
pingamizi zao pia na walioweka pingamizi.
No comments:
Post a Comment