Mwanariadha na mwanaharakati wa mageuzi
katika michezo, Wilhelm Gidabuday amethibitisha kuongoza timu ya wakongwe
wenzake katika mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Marathon yanayotarajia kufanyika
jumapili ya Machi 3, mkoani Kilimanjaro.
Gidabuday amesema wameamua kuja Kilimanjaro Marathon
mwaka 2013 kwa lengo la kuwaunga mkono wakimbiaji wa kitanzania na
kuhakikisha kuwa mbio za mwaka huu hazirudii makosa ya miaka ya
nyuma.
Amesema kuwa mbio za Kilimanjaro marathon ni mbio kubwa kuliko zote Tanzania na hivyo ni vizuri watanzania wakijionea ufahari wa kuandaa mbio kubwa kama hizi katika ardhi yao huku akiwashukuru waandaaji wa mbio hizi kwa jitihada zao kufanya mbio hizi kuwa za kimataifa zaidi.
Amewataja wanariadha wakongwe atakaoongozana nao,
wakiwemo wanaokimbia hadi hivi sasa, kuwa ni pamoja na Andrea Sambu ambaye
aliwahi kuwa bingwa wa dunia pekee Mtanzania katika mbio za nyika za dunia mwaka
1991, Faustin Baha Sule, ambaye ni mshindi wa medali ya fedha mbio za nusu
marathon 2000.
Wengine ni John Steven Akhwari aliyeiwakilisha nchi katika mbio kadhaa za nyika za dunia, Getuli Bayo, Michael Sarwatt, Thadeo Nada na Anthony Mwingereza ambao kwa pamoja wamewahi kupeperusha vyema bendera la Taifa.
Mimi naenda Moshi kumona huyu jamaa, ee bwana huyu mtu hatari lazima nimone, mwili kanyimwa lakini akili na ujasiri tele, namkubali sana akifuatiwa kwa karibu na Mike Wambura.
ReplyDelete