HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

28 February 2013

TENGA :NDIYE WAKULAUMIWA TULIPOFIKA "WAMBURA "

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg3grnLcdwE1Y4MuSkpyIej2OhMbtebHNF10hJS_Ubs2-PO-2_qXwBC-dnwA8Vncg6UOJubl3y9CuFpGmh70Qv6AWQYzVUP3f_yCXdFYAOMkBabdNX09EBGzZ8MhR0ZycajiLVfxUyStdk/s1600/Michael-Wambura1%5B1%5D.jpg 
KATIBU wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT), sasa TFF, Michael Wambura amemtaka  rais wa TFF Leodegar Tenga kuomba radhi wadau wa mpira wa mgiuu kuwa alikosea na alikiuka  katiba ya TFF.



Wambura aliyasema hayo leo alipozungumza na vyombo vya habari kwenye ukumbi wa Idaa ya  Habari (MAELEZO) na kudai kuwa Tenga anapaswa kuomba radhi kwa kukiuka katiba kwa  kufanya marekebisho ya katiba ya shirikisho hilo bila kuitisha mkutano mkuu ambao una mamlaka  ya kufanya mabadiliko ya katiba hiyo.

"Tenga aelewe mgogoro wote uliojitokeza ambao utaadhiri mpira hapa nchini atawajibika moja  kwa moja na watanzania tutamtwisha mzigo wa lawama kwa kuwa matatizo yanayojitokeza sasa   aliyafahamu mapema.

"Kwa vile serikali imeshafanya uamuzi ake nina lazimika kuamini Tenga na Kamati yake ya  utendajji wataiii na kutekeleza uamuzi huo, baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya TFF ni 

watumishi wa serikali akiwemo Magori -NSSF, Wallance Karia - Tamisemi, Ramadhan Nassib -NSSF, Athuman Nyamlani -Mahakama na Athuman Kambi - Tanroad hivyo kwenda kinyume na  maamuzi ya serikali itakuwa utovu wa nidhamu. "Wakati anajiuzulu BMT mwaka 2001 alijaribu kuwaonyesha watanzania kuwa yeye ni muumini  wa kufuata sheria na tararibu zilizopo na haya ni maneno aliyosema wakati akijiuzulu


 "Hatuna budi  kutekeleza majukumu yetu kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo kinyume chake ni vurugu,  pale tunapoona sheria yetu imepitwa na wakati na haifai inatulazimu tukubaliane na kuifanyia  mabadiliko kabla hatujaacha kuiheshimu." alinukuu Wambura na kuongeza "Ni wazi Tenga anafahamu kuwa kwenda kinyume na utaratibu halali uliowekwa wa mabadiliko ya  katiba ya TFF mwisho huleta vurugu kama ambavyo falsafa yake inavyomuelekeza, kwa mantiki  hiyo  anatulazimisha watanzania tuamini mkanganyiko huu uliopo sasa Tenga aliufahamu mapema  na alishiriki na kuruhusu hali hiyo itokee kwa maslahi yake binafsi.

Mwaka 2001 Tenga aliweka wazi moja ya sababu ambazo zilimfanya achie ngazi BMT ni akiwa ni  makamu mwenyekiti wakati huo ni kupinga uamuzi wa serikali kukubalina na fifa kuhusu undwaji  wa kamati ya mpito ya fat kwa madai kuwa kufanya hivyo serikali itakuwa imepoeza uwezo wa  kusimamia vyama vya michez nchini.

Akinukuu tena kauli ya Tenga aliyotoa mwaka 2001  "Kukubali kutekeleza agizo la fifa kama  ilivyoamuliwa na serikali ni kuzitelekeza taratibu na sheria za nchi, serikali imejivua madaraka ya  udhibiti wa vyama vya michezo vya kitaifa na kulikabidhi jukumu hilo kwa vyama vya michezo vya  kimataifa. Haiwezekani tufanye hivyo na hakuna nchi yoyote makini inayofanya hivyo.

Wambura alisema "Swali la kujiuliza Tenga huyu na yule wa wakati ule 2001  wanatofauti gani au  kwa kuwa sasa ameishaingia TFF na kuanza uswahiba na fifa na hviyo kuamua kuwasaliti  watanzania waliompigia debe kwenye uchaugzi wa 200, kwa kiwango alichofikia lazima aheshimu  na kuutetea uamuzi, imani na falsafa yake vinginevyo hataheshimika na kuaminika tena.

Aidha Wambura aliitaka TFFkuinusuru hali mbaya ndani ya shirikisho kwa kuwaangukia wadau  waliofungua kesi dhidi  yao kumalizana nje ya mahakama. TFF imeshitakiwa, Tanga na Mwanza ambapo walalamikaji wamefungua kesi za kupinga  kuenguliwa kushiriki Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Februari 24 Dar es Salaam kabla ya  kusimamishwa.

Hata hivyo Kamati ya Utendaji inakutana kesho, Dar es Salaam kujadili uamuzi wa serikali  kutoitambua katiba mpya ya TFF na kutaka mchakato wa mabadiliko kufanyika upya kabla ya  kuidhinishwa na serikali. "Nadhani muhimu kabla ya yote ni kwanza ikutane na walalamikaji nje ya mahakama na  kuwashawishi kufuta kesi walizofungua ili Fifa wakija wamalize mambo kirahisi," alisema  Wambura.
"Hakuna kitakachoweza kufanyika hata Fifa wakija. Kamati ya Utendaji ya TFF inaundwa na  wajumbe watano, ambao naamini wakikutana wanaweza kufanya uamuzi sahihi kwa maslahi ya  soka la Tanzania," aliongeza.
Lakini pia katika hali ya kunusuru soka la Tanzania, TFF iridhie kutekeleza uamuzi wa serikali kwa  kuitisha mkutano mkuu na kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi." Hatma ya uchaguzi huo itajulikana April 16 wakati Mahakama Mwanza itakapotoa hukumu ya kesi  ya mlalamikaji, Richard Rutambura aliyepinga kufanyika kwa uchaguzi huo mpaka kesi yake ya  msingi kupinga kuenguliwa kushiriki uchaguzi itakapoamriwa.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers