Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limesitisha ukamishna wa Hafidh Ali.
Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya
Afrika iliyokutana Januari 17 mwaka huu jijini Johannesburg, Afrika
Kusini.
Kwa
mujibu wa barua ya Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani kwa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ukamishna huo umesitishwa kwa vile
hadi sasa Shirikisho hilo halijapata ripoti ya mechi namba 78 kati ya
Comoro na Libya ambayo Ali aliteuliwa kuisimamia.
Hivyo,
ukamishna wa Ali umesitishwa hadi hapo CAF itakapopokea ripoti
kuhusiana na mechi hiyo ambayo ilikuwa ni kutafuta tiketi ya kucheza
Fainali za AFCON zilizofanyika mwaka huu nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment