Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa
Chama cha Wataalamu wa Tiba ya Michezo Tanzania (TASMA) uliochaguliwa
katika uchaguzi uliofanyika Februari 10 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TASMA walivyo na imani kubwa kwao katika
kusimamia tiba ya wanasoka nchini.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya TASMA
chini ya uenyekiti wa Dk. Mwanandi Mwankemwa aliyeibuka mshindi katika
uchaguzi huo kwa kura 18 dhidi ya 7 za aliyekuwa Mwenyekiti Biyondho
Ngome
Uongozi
huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha
shughuli za mpira wa miguu kwa kuzingatia katiba ya TASMA pamoja na
vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya TASMA chini ya Dk. Paul
Marealle na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo
unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Safu
nzima ya uongozi wa TASMA iliyochaguliwa inaundwa na Dk. Mwanandi
Mwankemwa (Mwenyekiti), Dk. Nassoro Matuzya (Katibu Mkuu), Sheky
Mngazija (Katibu Msaidizi), Dk. Juma Mzimbiri (Mhazini), Joakim Mshanga
(mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF) na Dk. Hemed Mziray (mjumbe wa Kamati ya
Utendaji).
Ukiondoa
nafasi ya Mwenyekiti, wagombea wengine wote hawakuwa na wapinzani.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti haikupata mgombea, hivyo itajazwa katika
uchaguzi mdogo utakaofanyika baadaye mwaka huu.
KILA LA KHERI AZAM, JAMHURI, SIMBA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linazitakia kila la kheri timu za
Azam, Jamhuri na Simba ambazo zinaiwakilisha Tanzania katika michuano ya
Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.
Azam
inacheza na Al Nasir Juba ya Sudan Kusini katika mchezo wa Kombe la
Shirikisho utakaofanyika Jumamosi (Februari 16 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Nayo
Jamhuri ya Zanzibar kesho itacheza na St. Georges ya Ethiopia katika
mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaofanyika Uwanja wa Gombani
kisiwani Pemba. Simba itacheza na Recreativo do Libolo ya Angola
keshokutwa (Februari 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment