HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

17 February 2013

HAKUNA UCHAGUZI TUNAANZA UPYA MMESIKIA


Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Deogratius Lyato alitangaza kusitisha zoezi la uchaguzi wa TFF kwasababu mchakato wa uchaguzi huo ulikumbwa na matatizo ya kikanuni ambayo hata hivyo hakuwa tayari kuyaweka bayana,  zaidi ya kusema kuwa yanatokana na ibara ya 10(5) cha kanuni za uchaguzi.
Kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini imesitisha zoezi la uchaguzi wa shirikisho hilo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni matatizo ya kikanuni.

Akitangaza kusitisha zoezi hilo mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Deogratius Lyato amesema kamati yake imepitia mchakato mzima wa uchaguzi wa shirikisho la soka nchini TFF na uchaguzi wa Tanzania Premier League Board(TPL Board) ili kujiridhisha kuwa mchakato mzima wa uchaguzi unakidhi kikamilifu matakwa ya kanuni za uchaguzi na katiba TFF.

 Kamati ya Uchaguzi ya TFF imebaini kuwa kuna matatizo ya kikanuni ambayo yanapaswa kuzingatiwa kwanza kabla ya kuendelea na mchakato wa uchaguzi.

Lyato amesema amesema kamati ya uchaguzi ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania kwa mamlaka ilinayo kwa mujibu wa Ibara ya 10(5) ya kanuni za Uchaguzi za TFF INASITISHA zoezi la uchaguzi wa Tanzania Primier League Board(TPL Board) na uchaguzi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF hadi hapo matatizo hayo ya kikanuni yatakapopata utatuzi.

Pia Lyato amesema kamati yake ya uchaguzi itawatangazia baadae tarehe mpya za uchaguzi wa Tanzania Premier League Board(TPL Board) na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania(TFF)

Kwa maana hiyo ni kwamba mchakato wa kampeni uliokuwa uanze kesho kwa mujibu wa kanuni ambayo inataka kampeni kufanyika katika kipindi cha siku tano sasa  hautakuwepo tena.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers