HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 September 2012

MMAREKANI KUFUNDISHA KIKAPU TZ


SHIRIKISHO LA MPIRA WA KIKAPU NCHINI  TBF LIMEPATA MAKOCHA WAWILI WA KIGENI KUTOKA NCHINI MAREKANI AMBAO WATAKUWA NA MAJUKUMU YA KUFUNDISHA TIMU ZOTE ZA TAIFA ZA WANAWAKE NA WANAUME NA PIA KUFUNDISHA MAKOCHA WAZALENDO NA PIA WATAKUWA NA JUKUMU LINGINE LA KUTOA USHAURI WA KIUFUNDI KWA TBF.
Makocha hao ni Abert Sokaitis ambaye atakuwa kocha ,mkuu ambaye ana uzoefu wa kufundisha kwa  miaka 24 na kwasasa ni kocha mkuu wa timu ya chuo kikuu cha post huko marekani katika jimbo la Connecticut.
kocha huyo atasaidiwa na Jocques L. Sconiers ambaye ana uzoefu wa miaka mingi ambaye pia ni kocha msaidizi wa chuo kikuu cha Post huko marekani katika jimbo la Connecticut.
makocha hao wote wana vyeti vya shahada ya juu kutoka vyuo vikuu mbalimbali  vya nchini Marekani na wanatarajiwa kuwasili nchini tarehe 21/09/2012 na kuanza mafunzo rasmi kwa timu zetu zote mbili kuanzia tarehe 22/09/2012.
Akiongea na waandishi wa habari makamu wa Rais wa TBF Phares Magesa amesema TBF imewateua makocha wasaidizi 4 watakao fanya kazi na waalimu hao wa kigeni.
makocha hao ni Everist J Mapunda, Leonard V Kwale, Angela Semw aiko na Bahati Mgunda ambao watatangaza vikosi vya timu ya taifa vya wanawake na wanaume mapema juma lijalo.
wakati huohuo michuano ya kombe la Taifa  imepangwa kuanza kutimu vumbi 20 mpaka 27 Octoba jijini Tanga ambapo TBF imetaka mikoa ianze kujiandaa ambapo vyama vya mikoa vimetakiwa kutoa msaada kwa timu zao ambapo pia wametakiwa kuthibitisha juu ya ushiriki wa timu zao.
Wakati hayo yakiwa hivyo Tanzania imekubaliwa kuandaa michuano ya kanda ya tano ya FIBA michuano ambayo ni mikubwa katika kanda ambayo inatarajia kushirikisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibout, Misri, Sudani na Sudani ya kusini.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika  jijini Dar es Salaam desemba mwaka huu.
Rockersport

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers