Chama
cha netiboli nchini kimetangaza uchaguzi wa chama hicho utafanyika
march 23 mkoani Dodoma ili kupata viongozi wapya baada ya waliopo
madaraka kumaliza muda wao.
Mwenyekiti
wa chaneta Anna Bayi amesema uchaguzi huo unafanyika kwa kufuata katiba
ya chaneta ambayo kwa sasa ni katiba kamili tofauti na miaka ya nyuma
walikuwa wakitumia rasim ya katiba.
Amesema
fomu zinaanza kutolewa mwezi wa pili tarehe 23 ambapo wagombea
watatakiwa kulipia fomu ya mwenyekiti na makamu wake pamoja na mweka
hazina laki moja na nusu wakati fomu ya mjumbe ni elfu hamsini.
Vyama
ambavyo ni wanachama wa chaneta wanatakiwa kulipa ada ya uwanachama ili
chama kiwe hai na kabla ya uchaguzi kutakuwa na mkutano wa wanachama wa
chaneta
No comments:
Post a Comment