Chama cha riadha tanzania (AT) kimesogeza mbele mbio za nyika na kimebadili pia sehemu ya kufanyia mashindano hayo .
Katibu mkuu wa chama cha raidha Tanzania Suleiman Nyambui amesema kuwa mashindano hayo yalitakiwa kufanyika mkoani kilimanjaro lakini sasa yatafanyika mkoani Morogoro March 10 .
Sababu kubwa ya kubadili tarehe na sehemu ya mashindano ni kupata muda zaidi wa kuchangisha kiasi cha Mil T 24m/- ambazo zinahitaji kwa ajiri ya mashindano hayo .
kubadilishwa kwa sehemu ya mashindano kutokana na kukosekana kwa eneo la kufanyia mashindano wakati itakuwa wazi na uwezekano wa kufanyia mashinadno hayo.
Nyambui
amesema kuwa ili ni jambo la kimaendeleo na litawapa fursa watu wa Morogoro kuona mashindano hayo .
“Tumeamua kusukuma mbele hadi mwezi March ,Tunatumaini itawapatia mikoa nafasi ya kujiiimarisha na sisi kutafuta vyanzo vya kupata fedha jumla ya shilingi mil 24 m/- ambazo zinahitajika kuandaa mahindano hayo ”,
Maafisa wa AT wamesema kuwa mashinadno yatatumika kuchagua wanariadha watakao shiriki mbio za nyika zitakazo fanyika Bydgoszcz
Poland mwezi March.
No comments:
Post a Comment