WAOMBAJI
uongozi kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliokata
rufani kupinga kuenguliwa kwenye kinyang’anyiro hicho wanaruhusiwa kuwa
na uwakilishi wa kisheria (legal representation) wakati wa kusikilizwa
rufani zao.
Uamuzi
wa kuruhusu mawakili kwenye usikilizaji wa rufani hizo mbele ya Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Idd Mtiginjola ni
kuhakikisha kila upande unapata haki.
Pia
Kamati ya Uchaguzi ya TFF ambayo ndiyo iliyosaili waombaji uongozi,
hivyo kuwa mlalamikiwa katika rufani hizo, nayo inaruhusiwa kuwa na
Wakili wakati wa usikilizaji wa rufani hizo.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF iliwaengua waombaji kumi na mbili wa uongozi kwenye
nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari 24 mwaka
huu jijini Dar es Salaam kwa kutokidhi matakwa ya kikatiba. Uchaguzi wa
TPL Board utafanyika Februari 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Waombaji
hao waliochujwa ni Omari Mussa Nkwarulo aliyeomba kuwania urais na
Michael Richard Wambura aliyejitosa katika kinyang’anyiro cha nafasi ya
Makamu wa Rais.
Wengine
waliochujwa wakiomba kugombea nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni
Abdallah Hussein Musa, Mbasha Matutu, Charles Mugondo, Ayubu Nyaulingo,
Nazarius Kilungeja, Eliud Peter Mvella, Farid Nahdi, Omari Isack
Abdulkadir na Shafii Kajuna Dauda.
Kwa
upande wa uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu aliyechujwa ni Christopher Peter
Lunkombe aliyekuwa akiomba nafasi ya ujumbe katika Kamati ya
Uendeshaji.
Mwisho
wa kukata rufani kwa waombaji uongozi walioenguliwa na wale walioweka
pingamizi kwa wagombea na zikatupwa ni leo (Februari 7 mwaka huu) saa 10
kamili jioni.
No comments:
Post a Comment