Mwanariadha mlemavu wa Afrika
Kusini Oscar Pistorius, anahojiwa na polisi kufuatia mauaji ya mpenzi
wake nyumbani kwake mjini Pretoria.
Kulingana na vyombo vya habari, mkuu wa polisi,
Sarah Mcira, aliwaambia wanahabari kuwa mwanamke aliyefariki nyumbani kwa
mwanariadha huyo alipigwa risasi kwenye mkono wake na kichwani.
Hata hivyo hali iliyosababisha mauaji hayo bado
haijulikani. Vyanzo vinasema kuwa Pistorius huenda alimuua mwanamke huyo
kimakosa kwa kudhania kuwa ni mwizi aliyekuwa amemvamia.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 26, alikuwa mwanariadha wa kwanza mlemavu kushiriki michezo ya Olimpiki.
Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye visa vingi vya uhalifu duniani na watu wengi wanamiliki silaha za kujilinda.
No comments:
Post a Comment