HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

5 March 2013

BEKI WA KUPASULIWA SHAVU MWANANYALA


 

 Beki Ladislaus Mbogo wa Yanga anatarajiwa kupasuliwa uvimbe wa kwenye shavu lake na madaktari wa hospitali ya Mwananyamala wakishirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam muda wowote kuanzia leo,.

Akizungumza  muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa Bora uliopo Kijitonyama, Dar es Salaam , daktari wa Yanga, Nassoro Matuzya amesema kuwa wanatarajia kumfanyia upasuaji katika shavu la kushoto beki huyo aliyejiunga na Yanga mwaka jana akitokea Toto Africans ya Mwanza.


Matuzya amesema kuwa tayari wameshafanya uchunguzi wa awali juu ya uvimbe huo na kwamba kinachosubiriwa ni ripoti ya madaktari bingwa wa Muhimbili kabla shughuli ya upasuaji haijafanyika.


“Upasuaji huo utafanyika kwenye hospitali ya Mwananyamala, nitampasua kwa kushirikiana na Dk Erick baada ya kupata majibu ya vipimo vyake ambavyo leo  vinatolewa na madaktari bingwa wa Muhimbili,” aliongeza Matuzya.


Matuzya aliendelea kueleza kuwa wameamua kuwashirikisha madaktari wa Muhimbili ili kujiridhisha zaidi kama hapatakuwa na madhara baada ya kumpasua mchezaji huyo.


“Tumeamua kumfanyia upasuaji baada ya kutueleza kuwa haifurahii hali ya kuwa na tatizo hilo,” alisema daktari huyo ambaye alipewa jukumu la kuiganga Yanga akirithi mikoba ya aliyekuwa daktari wa timu hiyo, Juma Sufiani aliyeondolewa baada ya kushindwa kusafiri na timu kwenda Antalya, Uturuki ambako ‘Wanajangwani’ waliweka kambi ya wiki mbili kujiandaa kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.


Mbogo ambaye alikuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha Toto kabla hajajiunga na vinara hao wa ligi, alifanya mazoezi ya jana ya mabingwa wa soka Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) kabla hajaenda Muhimbili kuchukua majibu ya vipimo vyake.


Baada ya kutoka hospitali jana mchana, Mbogo alithibitisha kupewa majibu ya vipimo vyake na madaktari wa Muhimbili huku Matuzya akisisitiza kuwa atatoa taarifa juu ya majibu ya vipimo hivyo baada ya kuyapitia.


"Ni kweli Muhimbili wameshampatia majibu. Tukishapitia ripoti yao ndipo tutakuwa na muda mzuri wa kueleza ni lini hasa upasuaji utafanyika na mchezaji atakaa nje ya uwanja kwa muda gani," alisema daktari huyo.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers