Mwamuzi kutoka Tunisia Slim Jdidi, ambaye alichezesha mchezo wa nusu fainali na kuonyesha uwezo Mmbovu kati ya Ghana na Burkinafaso katika michuano ya Mataifa ya afrika amefungiwa na shirikisho la mpira wa miguu afrika CAF
.
Jdidi's aliyechezesha mechi ameibua maswali kutoka kwa wadau wa soka baada kutoa malalamiko dhidi ya maamuzi mabaya aliyoyafanya .
Moja kati ya Tukio ambalo liliwashtua watu wengi ni kumtoa nje kwa kadi nyekundu katika dakika 117 Jonathan Pitroipa akimutuhumu kuwa alijiangusha huku marejeo ya picha Runinga zikionyesha kuwa mchezaji huyo alifanyiwa madhambi ya dhahiri katika box la timu ya ghana
Pia mwamuzi alikataa goli la dhahiri lililofungwa na pitroipa bila sababu za msingi
.
"Tulitegemea kiwango bora zaidi alisema katibu mkuu wa CAF Hicham El Amrani
Tutakuwa na mkutano kuzungumzia jambo hili hapo kesho kuhusu ishu ya " Pitroipa ."
Aidha Burkinafaso wana imanai kuwa caf itabadili adhabu ya pitroipa japokuwa itategemea na mwamuzi
Jdidi atawasilisha ripoti ya aina gani .
Kamati ya maandalizi haina uwezo wa kubadili maamuzi ya mwamuzi hadi atakapo ridhia mwenyewe mwamuzi
", aliongeza El
Amrani.
No comments:
Post a Comment