Pambano
la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Cameroon
(Indomitable Lions) lililochezwa jana (Februari 6 mwaka huu) na wenyeji
Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0 limeingiza sh. 148,144,000.
Fedha
hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 23,092 waliokata tiketi
kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh.
10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko
la Thamani (VAT) ni sh. 22,598,237.29, maandalizi ya mchezo sh.
58,000,000 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,340,900.
Nyingine
ni bonasi kwa wachezaji wa Taifa Stars sh. 18,831,864.41, asilimia 20
ya gharama za mchezo sh. 8,274,659.66, asilimia 15 ya uwanja sh.
6,205,994.75 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
sh. 2,068,664.92.
Asilimia
60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 24,823,978.98 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,241,199
ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
No comments:
Post a Comment