Mabingwa wa kombe la Kagame timu Young Africans leo imeendeleza
wimbi lake la ushindi katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom
baada ya kuichapa timu ya African Lyon jumla ya mabao 4-0, katika
mchezo uliofanyika jioni hii katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam.
Young Africans ambayo inaongoza ligi kwa kuwa na pointi
36 na mabao 33 ya kufunga, iliingia uwanjani kwa ajili ya kusaka pointi
3 muhimu ambazo imefanikiwa kuzipata.
Kikosi cha
mholanzi Ernest Brandts kiliuanza mchezo kwa kasi, na katika dakika 15
za kwanza washambuliaji wake Hamis Kiiza na Jerson Tegete walikosa
nafasi za wazi za mabao ya mapema, kufuatia kutokua makini katika
umaliziaji.
Jerson Tegete aliwaiunua mashabiki wa
Yanga katika dakika ya 21 baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza kwa
kichwa akimalizia pasi safi iliyopigwa na mlinzi wa pemebeni David
Luhende ambaye alipanda kuongeza nguvu mashambulizi.
Yanga
iliendela kuutawala mchezo na hasa sehemu ya kiungo, ambapo Haruna
Niyonzima, Athumani Idd Chuji, Frank Domayo waliweza kuitawala sehemu
hiyo ya katikati hali iliyopelekea wachezaji wa African Lyon kuutafuta
mpira kwa tochi.
Dakika ya 42, Jerson Tegete tena
aliiptaia Young Africans bao la pili kwa staili ya peke, baada ya
kuupiga kwa kisigino mpira wa krosi uliokuwa umepigwa na Haruna
Niyonzima na kumfanya mlinda mlango wa African Lyon Abdul Seif na
walinzi wake wasijue cha kufanya.
Saimon Msuva
alitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini mipira hiyo ilipowakuta
wafungaji hawakua katika nafasi nzuri ya umaliziaji hali iliyoplekea
kukosa mabao mengine ya wazi katika kipindi cha kwanza.
Kocha
wa African Lyon, Salum Bausi, akiwa katikati ya uwanja akiwatuliza
wachezaji wake kukubali kupigwa penati, waliyokuwa wakiigomea, huku
wakimzonga refa.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza Young Africans 2-0 African Lyon.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi na Yanga kuutawala mchezo hali iliyopelekea
kujipatia penati dakika ya 48 ya mchezo, kufuatia walinzi wa African
Lyon kuzidiwa na kiungo Haruna Niyonzima hali iliyowapelekea kumcheza
madhambi mchezaji huyo ndani ya eneo la hatari, mwamuzi aliamuru ipigwe
penati ambayo iilipigwa na Hamis Kiiza ambaye alikosa penati hiyo.
Kocha
wa Yanga Ernest Brnadts alifanya mabadiliko ya kuwaingiza Didier
Kavumbagu, Said Bahanuzi, na Nizar Khalfani ambao walichukua nafasi ya
Hamis Kiiza, Jerson Tegete na Saimon Msuva.
Mbadiliko
hayo yalizidi kuongeza kasi ya mashabuluzi langoni mwa African Lyon
kwani dakika ya 70, Didier Kavumbagu aliipatia Yanga bao la tatu kwa
mkwaju wa penati kufuatia mlinzi wa African Lyon Obina Salamusasa
kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Dakika ya
80 Nizar Khalfani aliipatia bao la nne ka ustadi mzuri wa umaliziaji,
akimalizia pasi ya Said Bahanuzi ambaye aliwazidi ujanja walinzi wa
African Lyon na kupiga krosi hiyo iliyowapita walinzi na mlinda mlango
Juma Abdul.
Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 4 - 0 African Lyon
Kocha
mkuu wa Yanga Ernest Brndts amesema anashukuru timu yake kupata kwa
ushindi katika mchezo wa leo, kipindi cha kwanza washambuliaji wangu
hawakuwa makini lakini kipindi cha pili timu ilibadilika sana hali
iliyopelekea kuutawala mchezo kwa kipindi chote na kuongeza mabao mawili
ya haraka.
Baada
ya mchezo huu wa leo kikosi cha Young Africans kitaendelea na mazoezi
yake kesho asubuhi katika uwanja wa Mabatini Kijitonyama ikiwa ni
maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya timu ya Azam FC februari 23
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans:
1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul, 3.David Luhende, 4.Nadir
Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman Idd 'Chuji', 7.Saimon
Msuva/Nizar
Khalfani, 8.Frank Domayo, 9.Jerson Tegete/Didier Kavumbagu 10.Hamis Kiiza/Sadi Bahanuzi, 11.Haruna Niyonzima
African Lyon: 1.Abdul
Seif, 2.Yusuf Mlipili, 3.Sunday Bakari, 4.Ibrahim Job, 5.Obina
Salamusasa, 6.Abdulehan Gulam, 7.Amani Kyata, 8.Mohamed Samata, 9.Idd
Mbaga, 10.Bright Ike, 11.Adam Kingwande
No comments:
Post a Comment