Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Majaliwa, amewataka wakuu wa shule za msingi na sekondari nchini kuanzisha program za michezo shuleni na kuzisimamia ipasavyo.
Majaliwa aliyasema hayo wakati wa siku ya mwisho ya ziara yake mkoani Singida wakati alipokutana na watendaji wa sekta ya elimu kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Waziri Majaliwa alikumbusha kuwa, serikali imesharudisha michezo shuleni na hivyo programu za michezo zinapaswa kupewa nafasi huku pia akizitaka halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji kuipa michezo kipaumbele kwa nia ya kuibua vipaji vipya kwa manufaa ya klabu na timu za taifa za michezo mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment