OFISA
 Maendeleo wa Kusini mwa Afrika wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa 
Miguu (FIFA), Ashford Mamelodi amewasili leo kwa ajili ya kufuatilia 
shughuli za maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Mamelodi,
 ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa shughuli za maendeleo nchini Tanzania 
tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo, pia amekuja kumtambulisha 
msaidizi wake, Patrick Onyango aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo hivi 
karibuni.
Wakiwa
 nchini, wawili hao wanatarajiwa kupata taarifa ya maendeleo ya mradi wa
 kuweka nyasi bandia kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, baada ya 
FIFA kuipa Tanzania mradi wa nne (GOAL Project 4) wa kuweka miundombinu 
kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu.
Mwanza
 ilipata mradi huo baada ya Halmashauri ya Jiji hilo kukubali masharti 
ya mradi huo ya kulipia nakisi ya fedha zinazolipwa na FIFA, ambazo ni 
sh. milioni 700. Mradi huo wa kuweka nyasi bandia Nyamagana utagharimu 
sh. milioni 900, hivyo nakisi y ash. milioni 200 italipiwa na Jiji la 
Mwanza.
Pia
 Mamelodi na Onyango watapata taarifa ya maendeleo ya Uwanja wa 
Gombani uliowekwa nyasi za bandia kwa msaada wa FIFA katika mradi wa 
GOAL Project 3; na pia kupata mikakati ya maendeleo ya TFF kwa mwaka 
2013, ikiwa ni pamoja na kozi na semina mbalimbali zitakazofanyika 
nchini mwaka huu.
Mamelodi
 na Onyango pia watapata taarifa ya maendeleo ya uboreshaji wa 
mashindano ya Copa Coca-Cola baada ya FIFA kuingia rasmi kwenye 
mashindano hayo mwaka jana kwa kuendesha kozi kwa walimu wa timu za 
kombaini ya mikoa na waamuzi.
Kwa
 sasa mashindano hayo yanashirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 
17, lakini FIFA inataka yahusishe umri mdogo zaidi ili kuendeleza soka 
ya vijana na kushirikisha kikamilifu shule. Maofisa hao wataondoka 
nchini Jumatatu asubuhi.
 
 
 
No comments:
Post a Comment