Salim Hadji amejiweka katika nafasi nzuri baada ya kuongoza kwa alama saba katika mashindano ya magari ya taifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam .
Hadji ambaye anatumia gari aina ya Mitsubishi Evolution alishinda mashindano hayo kwa alama 25 na kukaa kileleni na kujiweka katika nafasi nzuri hasa katika mkondo wa pili utakaofanyika Mwezi ujao mjini Moshi .
Aidha Rahim Suleiman amesema kuwa , kwa Hadji’ huu ni ushindi mkubwa kwake na hajawahi kushinda kwa alama hizo ,
Mshindi wa pili kwa sasa katika mashindano hayo kwa mujibu wa chama cha magari Tanzania ni Eric Cormac.
Klabu ya magari ya Arusha inaongoza kwa alama 18 ikifuataiwa na Marco Ferreira pia kutoka klabu hiyo hiyo .
Derva mwingine wa Dare s Salaam ambaye pia ameonyesha uwezo wa hari ya juu ni Fayaz Chandu ambaye ameweza kukusanya alama 12 baada ya kumaliza mpaka hatua ya mwisho ya mashindano .
Munir Farook alikuwa watano akikusanya alama kumi katika raundi ya mwsisho na wa mwisho ni Nizar Abba akiwa na alama nane .
Bingwa Mtetezi Dharam Pandya bado hajapata alama yoyote baada ya kutokushiriki mkondo wa kwanza .
No comments:
Post a Comment