Hali si shwari ndani ya klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba baada ya leo Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya wekundu hao Zakaria Hans Pope kubwaga manyanga.
Hans Pope ambaye amewasilisha barua yake ya kujiuzulu leo kwa mwenyekiti wa klabu hiyo,Ismail
Aden Rage amedai kuwa ameamua kuachia ngazi kutokana na mwenendo mmbaya wa timu hiyo ambayo
mwishoni mwa wiki iliyopita ilijikuta ikitolewa kwa aibu katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika
ilipokubali kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Recreative de Libolo ya Angola na kufanya kutolewa kwa
jumla ya mabao 5-0 baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kwenye uwanja wa taifa wiki mbili
zilizopita.

Klabu hiyo ya mtaa wa Msimbazi licha ya kuchemsha kwenye michuano ya klabu bingwa pia imeonekana
kusuasua katika Ligi Kuu ya Tanzania bara ambayo Yanga inashika nafasi ya kwanza katika msimamo
wa Ligi ikiwa na pointi 39 wakati Simba ipo nafasi ya tatu kitendo ambacho kinaiweka pabaya kutetea
ubingwa wake.
Sababu kubwa inayoonekana kusababisha mwenendo mbaya ndani ya kikosi hicho ni pamoja na usajili
mbovu ambao ulikua ukisimamiwa na Mwenyekiti huyo hali iliyosababisha kusajili wachezaji kwa
mamilioni ya pesa na baadae kuwaacha.
Miongoni mwa wachezaji aliowasajili na wengine kuacha ni pamoja na Kamonbil Keita,Patrick
Ochieng,kipa Dhaira,Emmanuel Okwi.
Hans Pope aliyekuwa jembe la usajili la Simba, amesema ameamua kuachia nafasi yake hiyo kutokana
na mambo yanavyokwenda.
Uongozi wa Simba kupitia kwa Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Geofrey Nyange 'Kaburu'
alidhibitisha kujiuzulu kwa Hans Pope.
"Hans Pope amejiuzulu na amewasilisha barua leo akimuandikia mwenyekiti ikieleza nia yake hiyo ya
kujiuzulu hata hivyo mwenyekiti kwa sasa hayupo nchini yupo India kwa matibabu."
Kujizulu kwake ni pigo kwa Simba ambayo imekuwa ikienda kwa mwendo wa kuyumba huku ikiwa
haina nafasi ya kutetea ubingwa.
Tangu kuingia kwake madarakani kiongozi huo ambae alikua akitumia mamilioni ya pesa katika
kusajili amejikuta akiingia katika mgogoro na uongozi wa timu hiyo pamoja na wanachama wao
wakidai imefanya usajili usio na tija kwa klabu hiyo.
Hans Pope aliyekuwa msaada mkubwa ndani ya klabu hiyo katika usajili , amesema ameamua kuachia
nafasi yake hiyo kutokana na mambo yanavyokwenda pamoja na kumaliza majukumu aliyokabidhiwa
na uongozi.
Alisema kufuatia kumaliza muda wake wa kuitumikia klabu hiyo ameona ni vyema akatoa nafasi kwa
wengine kushika nyadhifa hiyo kwa lengo la kuleta mabadiliko ndani ya klabu hiyo.
"Sijashinikizwa na mtu katika maamuzi yangu,nimeamua mwenyewe baada ya kuona muda wangu wa
kuitumikia Simba umemalizika kwani nataka kuwaachia na wengine,naamini kabisa majukumu
niliyopewa nimeyakamilisha kikubwa tuendelee kushikamana katika kuiendeleza timu hii"alisema
Hans pope.

Aliongeza"Kama timu inafanya vibaya ni heri kuwaachia wengine wajaribu kwani si vizuri lawama ni
bora,kifanye kitu kwa mafanikio na wanachama waridhike na mwenendo wa timu kwa hali hii sioni kama nastahili kuendelea kuingoza Simba".Makamu mwenyekiti wa Simba, Kaburu alisema uongozi umepokea barua ya kiongozi huyo na kwamba wataijadili na kuitolea maamuzi pale kamati ya utendaji ya klabu hiyo itakapokutana siku yoyote kuanzia sasa. Mtawala alisema Hans Pope alikua Mwenyekiti wa kuteuliwa hivyo wanafanya mawasiliano na Mwenyekiti wao aliyepo India kwa matibabu na watakaporuhusiwa kuzungumza lolote ndio watatoa kauli kama uongozi.

Simba ambayo imeondolewa katika hatua ya awali ya michuano ya kimataifa ya klabu bingwa Afrika
pia imejikuta ikiweka ubingwa wake rehani baada ya kufanya vibaya katika baadhi ya mechi zake za
ligi.Timu hiyo itashuka dimbani tena kesho kutwa Jumapili kuikabili Coastal union ya Tanga kwenye
uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

No comments:
Post a Comment