Baraza
la vyama vya soka Afrika mashariki na kati CECAFA limethibitisha kifo
cha aliyekuwa afisa habari wa baraza hilo Finny Muyeshi ambaye
amefariki dunia jana jioni.
Akiongea
na Rockersports katibu wa baraza hilo Nickolaus Musonye amesema kuwa
baraza lake limesikitishwa na kifo cha afisa habari wake ambaye amekuwa
mchapa kazi hodari ndani ya baraza hilo ambaye aliugua kwa muda mrefu na
hatimaye jana akafariki dunia.
Musonye amesema kuwa mazishi ya Muyeshi yatafanyika wiki ijayo.
Amesema
kwa CECAFA huo msiba mkubwa kwani alikuwa mstarabu na mwenye kujituma
muda wote katika kazi yake na kwamba pengo lake ni kubwa katika baraza
hilo.
No comments:
Post a Comment