HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

4 October 2012

CAF YAANZA KUMTAFUTA MFALME WA SOKA AFRIKA MWAKA 2012


Shirkisho la soka Barani afrika (CAF)  limeanza mchakato wa kutafuta mchezaji bora wa afrika kwa mwaka 2012.

huku jumla ya wachezaji 34 watakuwa wakiwania tuzo hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na mchezaji kutoka ivory coast  Yaya Toure.
Ambapo majina 32 ambayo yamepitshwa mpaka sasa wanacheza soka  ndani ya Afrika  Sherehe za kumtafuta Mchezaji Bora wa afrika zinazojulikana kama Glo Caf Gala 2012  zitafanyika Huko Accra Ghana  ,
Mwaka huu wachezaji wa tatu wanaogombania uchezaji bora ni wa zambia wawili  Rainford Kalaba na  Stoppila Sunzu kutoka klabu ya  TP Mazembe huku wakiungana na mchezaji toka Tunisia, Youssef Msakni kutoka klabu ya  Esperance katika uchezaji bora wa afrika ambapo tuzo hii imekuwa ikitawaliwa zaidi na wachezaji ambao hucheza soka nje ya afrika  
ambapo uteuzi wa majina uliegemea zaidi katika uwajibikaji wa wachezaji hao katika vilabu na timu ya taifa 
. CAF itatangaza wachezaji watano bora wanaogombania tuzo hiyo  wanaoacheza soka afrika mwishoni mwa mwezi oktoba kwa kupiga kula na kamati zinazotambulika kiukamalifu na CAF, majina ya wachezaji kumi bora na tano bora yatatumwa kwa vyama husika na kwa makocha wa timu za taifa ilikuchagua wachezaji watatu bora .
Aidha Tuzo zitakazogombaniwa katika sherehe hizo ni 

1.Timu ya Taifa ya Mwaka   

2.Timu bora ya wanawake ya Mwaka   

3.Timu ya Taifa ya Wanawake Ya Mwaka   

4. Klabu bora ya Mwaka 

5.Mchezaji mwenye kipaji kichachovutia   

6. Mkufukunzi Bora wa Mwaka 

7. Mwamuzi Bora wa Mwaka 

8. Tuzo ya Heshima kwa wachezaji wa Zamani 

9. Zawadi ya Ubinadamu kiwanjani 

10. Zawadi  Kwa taasisi au mtu ambaye amechangia maendeleo ya soka afrika au Duniani .

11. Kikosi bora cha Afrika 

Tuzo Kwa  Mchezaji bora wa afrika na kwa Mchezaji Bora afrika anayecheza soka ndani ya afrika .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers