Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania JK |
“Lazima
tutazame vilabu vyetu hapa Nchini Vinaongozwa zaje, wengi wetu tunafahamu
kuwa haviongozwi vizuri huo ndio mzizi
wa fitina bila kulitazama hilo hatutaweza kusonga mbele hadi mwisho wa Dunia “
Leo nimeona tutazame kwa undani kidogo kuhusu matatizo
yanayofanya Nchi yetu ya Tanzania kushindwa kufanya vizuri kimataifa ! wengi
wetu huwa tuna majibu rahisi katika maswali magumu
lakini hapa lazima tutafakari kwa kina tunashidwa kwa kiasi gani ama nini kinatufanya tushindwe
kufanikiwa katika Nyanja ya kimataifa ?
Moja kati ya mambo yanayoharibu soka au michezo kwa taifa la Tanzania
Ni mfumo wa uendeshaji wa michezo yenyewe, tuanze na vilabu vya soka ambapo kwa
nchi kama ya Tanzania kama hujazungumzia simba na yanga bado haujazungumzia soka
la Tanzania hapa nadiliki kusema hawa ndio wachawi wanaoharibu soka lote la Tanzania.
Tangu Rais mwinyi aliposhuhudia simba inafungwa nyumbani na stela Abidjan ya
ivory coast aliibatiza jina la kichwa cha mwendawazimu hii sio tu kiwanjani kuanzia klabu husika
mpaka na uongozi mzima .
Kwa Takriban muongo mmoja uliopita klabu za simba na yanga
zimekuwa kwenye migogoro isiyokwisha tena chaa ajabu imekuwa ikija kwa
kupishana pishana leo simba kesho yanga swali la kujiuliza wanaoongoza vilabu hivi
wanajua hata ABC ya uongozi kwanini imekuwa kero kila kukicha simba na yanga na
vilabu hivi vimekuwa vikiambukiza na timu nyingine katika za ligi hiyo ambavyo ni
vya kiraia kwa muongo huu mmoja,
sikuwahi kusikia Timu inayomilikiwa na jeshi
kuwa na mgogoro pengine inatokana na aina ya uongozi walionao .
Klabu za simba na yanga hutegemea sana wachama ambao swala
kufungwa huwa halipo kabisa katika akilizao kana kwamba wao wameandikiwa
kushinda tu au kutoa suluhu kitu ambacho sio kweli kwani hata Brazil hufungwa
kwani ndio timu pekee iliyotwaa ubingwa wa dunia mara nyingi zaidi .
Pengine ifike mahali kubadilisha mfumo wa aina ya wanachama kwani
aina ya mfumo wanachama wa simba na yanga ninamashaka nao lakini inawezekana wanalipa
mamiliano ya shilingi ndio maana wanaskia uchungu sana timu inapofungwa lakini
kwa kumbukumbu nilizonazo pesa wanayolipa haizidi hazidi hata shilingi elfu
mbili mia tano.
Ni mara chache sana kusikia vilabu vya ulaya kuwa na migogoro
hata sehemu za afrika kama afrika kaskazini, kusini mwa afrika na maghalibi
lakini kwa Tanzania haupiti Mwaka utaskia kelele kibaya zaidi unaweza
kuchaguliwa kwa kura nyingi lakini mwisho wa siku hukaonekana hauna maana hata
kidogo hizo ndizo simba na yanga .
Ukiachia simba na yanga vilabu vingi vianyoshiriki ligi Tanzania
au hata visivyoshiriki ligi Tanzania vina kabiliwa na tatizo kubwa la kiuchumi
ukitazama kiuzamini wazamini wengi hukimbilia kuvizamini vilabu hivyo hivyo
ambazo haviishi migogoro je kuna uwezekano wa pesa za wazamini hawa zikawa
zinaanzisha migogoro vilabu hujazwa mapesa na kuwa na nguvu kiuchumi na
hupambana na timu ambazo wakati mwingine nauli za kusafiria havina kabisa .
Tangu viwanda kadhaa vife au kushindwa kujiendesha timu zao
ushindani wa soka na michezo mingine umekufa kabisa mfano mzuri kiwanda cha
ushirika cha mkoani Kilimanjaro kilikuwa kikimiliki timu ya ushilika ya moshi.
Lakini tangu kiwanda kife na timu nayo imekufa viwanda vingi vimeshindwa
kuendesha timu kama sigara ambao walikuwa na timu ambayo iliwahi kushiliki hata
mashindano ya kimataifa , zipo timu nyingi za mashilika ya umma
ambayo ya leo mashilika husika na timu zake zimekufa lakini kikubwa
kinachooneka ni aina ya uongozi wa viwanda na vilabu husika kushindwa
kuendesha timu.
Jambo la msingi apa vilabu vya soka na vyama vimeshindwa
kupata viongozi sahihi wa kuongoza
taasisi hivi na sio vilabu hata serikali nayo imeshindwa ,kwa mfano simba na Yanga zimekuwa zikitumia mamilioni ya shilingi
kusajiri wachezaji walioshindikana nchini mwao ambao wachezaji hao wameshindwa kuzisaidi
simba hata kufika robo fainali ya klabu bingwa afrika kama sio kombe la shirikisho.
Mapesa wanayotumia kununua wachezaji kwa muongo mmoja yangeweza kabisa
kutengeneza mradi wa ukuzaji wa vipaji vya watoto lakini yote haya
yanasababishwa na mifumo iliyoooza ambayo hata Mbwa hawezi kunusa Rais kikwete
aliwahi kusema katika ziara ya kombe la dunia kuwa
“Lazima tutazame vilabu
vyetu hapa nchini Vinaongozwa zaje wengi wetu tunafahamu kuwa haviongozwi vizuri huo ndio mzizi wa fitina
bila kulitazama hilo hatutaweza kusonga mbele hadi mwisho wa Dunia “
Naam ipo
haja ya kuutafakari usemi huu lazima tutazame mifumo ya uongozi wa vyama husika
tuweke mifumo mipya itakayoweza kubuni mbinu za kuleta maendeleo kisoka na
michezo mingine bila hivyo ,Tanzania itapitwa hata na sudan kusini ambao ndio
taifa jipya katika soka afrika.
No comments:
Post a Comment