HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

26 March 2013

La Paz KIWANJA KILICHOPO MILIMANI BOLIVIA KINACHOZIPA TABU KLABU ZA NJE YA BOLIVIA NA TIMU ZA TAIFA

 

Moja kati ya jambo kubwa duniani ni kukumbana na timu ya soka ya Bolivia katika uwanja wao wa Nyumbani wa La paz  karibu timu zote zenye bora katika Uwanja huu ziliishia kukung'utwa hasa zinazotoka nje Nchi hiyo kutokana na eneo husika na hari za hewa japokuwa wiki hii ilipata balaa la kukung'utwa bao tano sifuri dhidi ya Colombia katika kufuzu fainali za kombe la dunia huko Brazil huku magoli ya Colombia yakifungwa na


  • Macnelly TORRES (20')
  • Carlos VALDEZ (49')
  • Teofilo GUTIERREZ (62')
  • FALCAO (86')
  • Pablo ARMERO (90'+3)  Lakini kwa upande mwingine hari ya kiwanja ambacho colombia ilitumia kina tofauti sana na Cha la paz ukitazama kiwaja hiki kiko juu ya vilima vya ambapo kadiri unapokwenda juu hewa huwa nyepesi zaidi kiasi cha kuwafanya wachezaji kushindwa kupumua vizuri na kushindwa  kucheza soka inavyotakiwa na hii huchukuliwa kama faida kwa wenyeji kwani siku wanapocheza na timu ambazo zinatoka eneo tofauti huishia kuchezea mvua za magoli pindi zinapocheza kwenye uwanja huo
  •        
  •  Hari hii iliifanya fifa kufungia baadhi ya viwanja kuchezea soka hasa katika viwanja vya mtindo huo lakini ilishindwa baada ya rais wa Bolivia Evo Morales kusimama kidete kugomea shinikizo la fifa kutaka kuvifungia viwanja hivyo visitumike katika soka hasa la kimataifa kiwanja kipo mita 2,500 na futi
    8,200 kutoka usawa wa bahari kitu ambacho hufanya hewa kuwa nyepesi sana katika upumuaji hasa kwa wachezaji.
  •  
  •  lakini kutoka na nchi zenyewe kijiografia zilivyo hulazimika kutengeneza viwanja katika maeneo kama hayo baada  ya kukosa sehemu mmbadala za kutengeneza viwanja husika. Diego Maradona aliwahikuchezesha timu yake dhidi ya Timu rais wa nchi hiyo katika kupingwa kufungiwa kwa viwanja hivyo na alikandamizwa mabao sita kwa moja alichoamua kufanya ni kupongeza wachezaji wa bolivia kuanzia wandani hadi benchi la ufundi.   
  •  Maeneo mengi ya nchi ya Bolivia ni ya muinuko kwa hiyo timu nyingi za kwao hupata faida kwa hari ya hewa ya eneo hilo na timu ngeni huishia kufungwa kwakuwa hawajazoea hari ya hewa ya eneo hilo na timu nyingi zimekuwa zikichezea mikong'oto japokuwa na ubora wao kuwa mzuri . 

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers