Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewasilisha rasmi maombi ya kuonana
na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara
ili kuzungumzia uamuzi wake wa kutengua usajili wa Katiba ya 2012.
Maombi
hayo yaliwasilishwa rasmi Wizarani jana (Machi 4 mwaka huu) ambapo TFF
imependekeza kikao hicho kifanyike keshokutwa (Machi 7 mwaka huu) au
Machi 13 mwaka huu.
Kamati
ya Utendaji ya TFF iliyokutana Machi 2 mwaka huu kujadili tamko ya
Waziri kutengua matumizi ya Katiba ya 2012 ndiyo iliyopendekeza kikao
hicho kwa lengo la kusikiliza upande wa TFF katika suala hilo.
No comments:
Post a Comment