HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

7 March 2013

WANALIZOMBE ,MAJI MAJI YA RUVUMA YALAMBA MILIONI MBILI KUTOKA HOSPITALI YA PERAMIHO


 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdXC-iEZ8dACbfLubznUvmMzHrYmoyCoTE_uFBc-htmMCYIA2_-Ya68UApH2qucIifFM86RAwl3_wr9COuUGY0wM00pa_jpgIN-S4G8w_CQQ37uYc7W-Q1uFde8tdogmd9pX7nk6KdkWe8/s320/peramiho+hospital.jpg

 Klabu ya Majimaji ya Songea imechangiwa fedha taslim Sh. milioni 2 na Hospitali ya Misheni ya Peramiho inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Abasiya ya Peramiho wilayani Songea kwa ajili ya kujiimarisha zaidi katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mechi zao za Ligi Daraja la Kwanza.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo ofisini kwake, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Misheni ya Peramiho, Dk. Venance Mushi, amesema kuwa uongozi wa hospitali yao ulipokea pendekezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea,   Joseph Mkirikiti la kutaka klabu ya Majimaji iungwe mkono kiuchumi kwani  inakabiliwa na changamoto nyingi huku ikiwa bado inashiriki ligi.


Mganga hiyo amesema kuwa kufuatia rai hiyo, wao waliridhia kuisaidia fedha Majimaji kwa nia ya kuona kuwa inawakilisha vyema mkoa wa Ruvuma, kwani wao pia ni wadau wa maendeleo ya michezo.


Akipokea msaada huo, Mwenyekiti wa Majimaji, Abdallah Milanzi, ambaye alikuwa ameongozana na viongozi wenzake kadhaa wa klabu akiwamo katibu  mkuu, Zacharia, aliushukuru uongozi wa hospitali hiyo na kusema kuwa fedha walizopewa zitawasaidia kujiandaa vyema na michezo mingine iliyobaki ya ligi daraja la kwanza. Hivi sasa wamebakiwa na mechi za nyumbani tu kumalizia ligi hiyo.


Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Ruvuma (Faru ), Golden Sanga, aliwataka wadau wengine wa michezo mkoani humo kuiga mfano wa Hospitali ya Misheni ya Peramiho katika kuiunga mkono Majimaji ili hatimaye itimize lengo lake la kurejea katika ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers