Timu ya soka ya Juventus ya Italia imemaliza ndoto za timu ya soka ya Celtic' kutoka uskochi za kutaka kuchukua ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kuwafunga kwa jumla ya mabao matano kwa sifuri .
Celtic ilianza mchezo kwa kasi baada ya Joe Ledley' kuonyesha uhai golini mwa Juve lakini Alessandro Matri na Fabio Quagliarella' walizima kabisa ndoto za Celtic baada ya kila mmoja kufunga goli katika kila kipindi .
Efe Ambrose alipoteza mpira baada ya kupiga kwa kichwa ,
Andrea Pirlo na Arturo Vidal walimtengenezea nafasi Quagliarella na kuifungia Juve' goli la pili .
Timu ya soka ya Paris St-Germain imeingia katika hatua ya Robo fainali kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 18 baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja dhidi Valencia katika uwanja wa Parc des
Princes na kufuzu kwa jumla ya magoli 3-2 .
Wageni wa mchezo huo walihitaji magoli mawili ya ziada ili waweze kusonga mbele na walianza vizuri baada ya , Jonas' kufunga goli safi lililoipa matumani Valencia .
Lakini Ezequiel Lavezzi alisawazisha ,na kuwaweka valencia katika wakati mgumu zaidi na walishindwa kabisa kupata goli la pili .
David Beckham hakucheza mechi hiyo na tangu ajiunge na timu hiyo amecheza mechi tatu japokuwa alikuwa amekaa katika viti vya wachezaji wa akiba .
Mchezaji huyo wa zamani amecheza mechi katika kikosi cha kwanza mara moja na amecheza mara mbili kama mchezaji wa akiba tangu ajiunge na Ancelotti'.
No comments:
Post a Comment