HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

5 March 2013

ZFA YAKUBALI MAKUNGU KUACHIA NGAZI YAMSHUKURU KWA KILA JAMBO KUPATA RAIS MWINGINE NDANI YA SIKU TISINI



 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgNYLwZsydR_lG6LNDFEn8tUyRZBzeZYIehGyw04sm3nTanADZV3G3kA9hvqNv33ronO9P1lvL8CPUBJrRKFWzlVhbYPDeLDC7owCcasMLks_0kUZabbo0Ol9SBMXthiHUktOZK6Gb3JDM/s640/amani+makungu.jpg
 Kamati ya Utendaji ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Kimeridhia  Maombi ya Aliyekuwa  Rais chama hicho , Aman Ibrahim Makungu kuachingazi nafasi hiyo.
Katika Barua iliyoandikwa na ZFA Machi 4, mwaka huu,  , iliyoisainiwa na Makamu wa Rais Kisiwani Unguja, ambaye pia ni Kaimu Rais wa ZFA kikatiba, Alhaj Haji Ameir, ikiwa na Kumbukumbu namba. ZFA/PRESIDENT/VOL.11/05.

Barua hiyo inasomeka  Kamati ya Utendaji ya ZFA Taifa, imekaa na kujadili kwa kina ombi la kujiuzulu kwa Makungu, na kutafakari kwa makini na hatimaye kufikia uamuzi wa kulikubali ombi hilo.

 ZFA Taifa imemshukuru Aman Makungu kwa msaada wake alioutoa huku wakimuomba aendelee kuwa na chama hicho wakati wowote atakapohitajika.
Nakala za barua hiyo zimetumwa kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo la Zanzibar pamoja na Msaidizi Katibu ZFA Kisiwani Pemba.

Kwa mujibu wa Katiba ya ZFA, sasa ni wazi kuwa kunalazimika kufanyika uchaguzi mwingine ndani ya siku 90.
Itakumbukwa kuwa miezi miwili iliyopita, Rais wa ZFA, Aman Ibrahim Makungu aliandika barua ya kuomba kujiuzulu nafasi hiyo kwa kile kilichoelezwa katika barua hiyo kuwa ni 

kuchoshwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho wasiotaka mabadiliko huku wakionekana kuwagawa baadhi ya wajumbe wa ZFA kwa kisingizio cha U-Unguja na U-Upemba, 
ambapo Kamati ya Utendaji ya ZFA Taifa walilikataa ombi hilo kwa madai kuwa litachangia kurejesha nyuma soka la Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers