Ndoto za Manchester United's kutwaa ubingwa wa ulaya zimemalizka kwa mjadara mkubwa huku kocha Man u Sir Alex Ferguson na wachezaji wakikiona kiwanja cha OT ni Kikubwa kuliko wakati mwingine.
United walionekana tayari wameanza kuingia hatua ya Robo fainali mara baada ya kipindi cha pili Kuanza huku Real Madrid's ikijitia matatani mara baada ya Sergio Ramos's kujifunga mwenyewe na kuipa goli United ambalo ilikuwa likichagizwa na sare ya goli moja kwa moja katika mchezo wa kwanza uliofanyika Bernabeu.
Lakini mchezo ulibadilika baada ya Mwamuzi kutoka Uturuki Cuneyt
Cakir's Kumlima kadi nyekundu Luis Nani baada ya kumchezea vibaya Mchezaji Real Madrid Alvaro Arbeloa katika dakika ya 56 - kadi ambayo iliwanyong'onyesha wachezaji wa United .
Vijana wa Jose Mourinho's , waliongeza bidii , na kutumia pengo la hilo ambapo mchezaji wa zamani na kiungo wa Tottenham Luka Modric na kijana wa zamani wa Timu hiyo Cristiano Ronaldo walitumia dakika sita kusawazisha na kufunga goli la ushindi na kusonga mbele katika hatua Robo fainali .
Baada ya luis Nani Kupewa kadi nyekundu Ferguson's alinoneka kuto kuamini kinachotokea na kumshutumu mwamuzi kuwa hakutenda haki baada kutolewa mchezaji wake .
Mourinho sasa atakuwa analisaka taji la tatu la ligi ya mabingwa barani ulaya akiwa na klabu tatu tofauti wakati Manchester utd wanatakiwa kujikita katika makombe ya nyumbani ambapo jumapili watakuwa wakipambana na chelsea katika kombe Fa huku wakiwa wanaongoza alama 12 dhidi ya bingwa mtetezi Manchester city .
Huenda mwaka huu ukawa kama 1996, ambapo England haikuwa na timu
yoyote kwenye hatua ya robo fainali, kwani Chelsea na Manchester City
walishatolewa na Arsenal wapo ukingoni wanapoelekea Ujerumani wiki
ijayo.
Baada ya mechi Rio Ferdinand alimwendea mwamuzi na kujidai kumpigia makofi kana kwamba anampongeza, bila shaka kuonesha kuudhiwa na uamuzi wake wa kumpa kadi nyekundu Nani, na pengine kuwanyima penati kadhaa walizodhani walistahili.
Katika mechi nyingine, Borussia Dortmund wamefanikiwa kutinga robo fainali, baada ya kuwachabanga Shakhtar Donetsk mabao 3-0, ambapo wamevuka kwa jumla ya mabao 5-2

Borussia Dortmund 3
Felipe Santana 31′ Goetze 37′ Blaszczykowski 59′
Shakhtar Donetsk 0
-
- FT 90 +2
Borussia Dortmund 3
Felipe Santana 31′ Goetze 37′ Blaszczykowski 59′
Shakhtar Donetsk 0
-
- FT 90 +2
- HT 2-0
- (agg 5 - 2)
No comments:
Post a Comment