HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

19 April 2013

Faustine Mussa na Joseph Daudi KUSHINDANA MASHINDANO YA DUNIA YA RIADHA HUKO MOSCOW ,URUSI



Wanariadha Faustine Mussa na Joseph Daudi wa mbio ndefu za marathon wamefuzu kushiriki mashindano ya riadha ya dunia yatakayofanyika Agosti 10 hadi 18 jijini Moscow, Urusi.

Katika mashindano hayo yanayoshirikisha wanariadha wanawake na wanaume kutoka nchi mbalimbali duniani, Tanzania inatarajiwa kupeleka wanariadha zaidi ya watatu endapo watafikia viwango vinavyotakiwa katika mashindano hayo.

  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha (RT), Suleiman Nyambui, amesema wanariadha hao wamefuzu kutokana na viwango walivyoonyesha wakati wakiwania kushiriki michezo ya Olimpiki.

"Tayari tuna uhakika wa kuwa na wanariadha wawili wenye sifa ya kushiriki katika mashindano ya dunia kwa mbio za marathon... sasa bado tunasubiri kupata washiriki watakaofuzu kwa  mbio za mita 5,000 na 10,000," alisema Nyambui.

Aliwataja wanariadha wanawake ambao RT inatarajia kuwa watafikia viwango vya kufuzu kwa michuano ya dunia kuwa ni pamoja na Zakia Mrisho (mita 5,000), Sara Ramadhan, Jacqueline Sakilu na Mary Naal wanaokimbia mita 10,000.


No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers